WAZIRI wa Afya , Ummy Mwalimu ameiagiza bohari Kuu ya dawa(MSD), kuweka nembo ya GoT dawa zote zinazoenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameiagiza bohari Kuu ya dawa(MSD), kuweka nembo ya GoT dawa zote zinazoenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya za serikali ili kuepusha uchepushwaji wa dawa hizo.
Waziri Ummy Mwalimu
Pia amesema Serikali itahakikisha inanunua dawa za kuhifadhi maiti kutoka kwa wazalishaji kwa bei rahisi kwani kwa sasa ni ghali.
Waziri Ummy meyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za afya zinazotolewa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala(Amana) jijini Dar es Salaam.
Amesema ameridhishwa na utoaji huduma huku changamoto ya upungufu wa watumishi ikiwa bado ipo na kwamba wagonjwa takribani 800 wanazuiwa hospitalini hapo.
"Madaktari waendelee kuchapa kazi kwa kufuata miongozo kanuni za Wizara ya Afya...dawa tumeona zipo lakini hazina nembo ya serikali ili tuweze kusimamia vizuri upatikanaji wa dawa,"amesema.
Amesema MSD ihakikishe kuwa dawa yoyote inayonunuliwa kwa fedha za serikali lazima iwe na nembo ya Serikali(GOT) ili kuepusha uchepushwaji wa dawa kwenda maduka ya dawa binafsi.
Amefafanua kuwa hospitali hiyo ina asilimia 80 ya dawa muhimu na kwamba amejiridhisha uwepo wa dawa muhimu 135.
Amesema serikali itahakikisha wananunua dawa za kuhifadhi maiti kutoka kwa wazalishaji kwa bei rahisi ili kupunguza gharama kwa wananchi.
"Tutakuja kwa bei elekezi tukishazinunua kutoka kwa wazalishaji ili waweze kupubguza malalamiko ya wananchi,"amesema.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Meshack Shimwela amesema asilimia 60 ya wagonjwa wanaowahudumia hospitalini hapo hawana rufaa huku akitaka wagonjwa kufika kwa rufaa ili kuongeza ufanisi.
"Sasa ni wakati umefika wagonjwa waje kwa rufaa ili ufanisi uweze kuongezeka na daktari aweze kuona wagonjwa ambao kweli wanauhutaji wake, "amesema.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments