Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma(PICHA NA MTANDAO)
Na Mwandishi Wetu
Baada ya waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kwenda Ikulu kuonana na Rais Magufuli na kupongeza baadhi ya mambo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano, kuna mengi yamezungumzwa kwenye mitandao na watu mbalimbali wa chama chake na hata vyama vingine.
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma ameona kauli za baadhi ya watu kushtushwa na kitendo cha Edward Lowassa kumpongeza Rais Magufuli ni kitendo cha kushangaza kwani viongozi hao wawili ni viongozi wanaojali maslahi ya wananchi.
Msukuma amesema kuwa kitendo cha kiongozi huyo kwenda Ikulu na kuzungumza na Rais Dakta John Magufuli ni kitendo cha busara kwani kitendo cha kumpongeza Rais ni kitendo cha ukomavu wa siasa za Tanzania.
Aidha mbunge huyo wa Geita vijijini amemuomba Edward Lowasa kuendelea kukaa katika chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kwani yeye mwenyewe ndio aliamua kujiunga na chama hicho.
Edward Lowasa jana alimtembelea Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam na kumpongeza kwa jitihada anazozifanya za kuliongoza taifa.
Comments