Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba amehaidi kumalizia mifuko 200 ya saruji na nondo 100 ili kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kata ya Kinampanda
Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba magharibi mkoa wa Singida amehaidi kumalizia mifuko 200 ya saruji na nondo 100 ili kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kata ya Kinampanda ambayo imekosekana kwa miaka mingi.
Waziri Nchemba amezungumza hayo baada ya kufika nakujiona hali ya kuridhisha ya ujenzi wa zahanati ya kata ya kinampanda ambao unafadhiliwa na ofisi ya mbunge wa jimbo akishirikiana na wananchi ambao wanachangia ujenzi huo.
“Kwa hatua ambayo mmeshafika hatuko mbali sana wiki ijayo nitashuhulikia tupate saruji na nondo na nitaongea na mkandarasi na vijaana wengine wapenda maendeleo wawepo hapa ndani ya wiki mbili wawe wameshafika juu na tunapofika maliza mwaka wa fedha tuwe tushakamilisha ujenzi,” alisema waziri Nchemba
Waziri Dkt. Nchemba yupo jimboni kwa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ambayo inafadhiliwa na ofisi ya mbunge akishirikiana na wananchi wa jimbo lake, miradi ambayo inaendelea kwasasa na ujenzi wa hosteli 22 za wasichana katika kata zote, zahanati na visima vya maji zaidi 75 vya kisasa.
Comments