SYSTEMS
TAMASHA la uchangiaji damu Salama lililoanza kufanyika jijini Dar es
Salaam juzi katika Wilaya ya Ubungo na jana kuendelea katika Wilaya
nyingine ya Ilala katika stedi kuu ya mabasi ya mwendo kasi Jijini
Dar es Salaam imeelezwa limefanyika kwa mafanikio.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana jijini hapa mratibu wa
tamasha hilo Bw.Prosper Magali kutoka kampuni ya Ensol Energy with a
smile ya jijini Dar es Salaam iliyojitokeza kudhamini shughuli hiyo
ambapo alisema kuwa lengo kubwa la kufanya tamasha hilo linafanyika
hili kuchochea msukumo wa hiari wa watu kujari maisha ya watu kujitokeza
kuchangia damu.
Alisema kuanzia mwanzo wa siku ya kwanza jumla ya chupa za damu
91 zilipatikana kwa watu waliojitokeza na hadi kufikia jana mchana
kulikuwa na jumla ya chupa 50 zilizopatikana ambapo zoezi hilo lili
kuwa bado likiendele.
"Tunaomba wananchi wajitokeze kuwa katika hali ya kuchangia damu
kwani kwa kufanya hivyo tunaokoa maisha ya watu sehemu mbali mbali
nchini wanaokuwa na maitaji ya kuongezewa damu,"alisema Prosper.
Prosper alisema kampuni yake imekuwa ikidhamini mpango huo baada ya
kuona hupo umuhimu wa kufanya hivyo kwa kuokoa maisha zaidi ya wanadamu
wanaokuwa wakiitaji damu.
Naye Fatuma Mtunga ambaye ni Afisa uhamasishaji toka mpango wa damu salama
alisema kuwa katika zoezi hilo walilenga hasa kufikisha takribani chupa
za damu takribani 450,000 kutoka kwa watu watakao jitokeza kuchangia.
Kampuni wadhamini wa tamasha hilo Ensol Energy with a smile waliojitolea kujihusisha
na mpango huo wa kudhamini ilikuhamasisha watu kuchangia dama kampuni yao
hiyo inajuhusisha na mambo ya uuzaji wa sola ambapo maduka yao yanapatikana
Ubungo Plaza .
Comments