Wanafunzi wa chuo cha DUCE wanaojitolea kufundisha masomo ya Sayansi ya hesabu katika shule za sekondari Na msingi zilizopo ndani ya wilaya ya Temeke wamemuomba Rais kuwawezesha kupata hela ya nauli ili waweze kufikia shule zote zilizopo ndani ya mkoa wa Dar es salaam.
Akiongea kwa niaba ya vijana wenzake, mwanzilishi na mratibu mkuu wa zoezi hilo Mr. Emijidius Cornel amesema kuwa walianza wakiwa vijana 10 lakini mpaka Sasa wamefikia vijana 400.
Pia amesema kuwa mpaka Sasa wamefikia shule 10 ndani ya wilaya ya temeke na kuongeza kuwa lengo lao kubwa ni kufikia shule zote ndani ya mkoa wa Dar es salaam ili waweze kusaidia watoto hasa kwa upande wa masomo ya sayansi ambapo ufaulu unaonekana kusuasua.
"Tumefikia shule 10 ndani ya wilaya ya temeke mpaka sasa lakini lengo letu ni kufikia shule zote zilizopo ndani ya mkoa wa Dar es salaam" amesema Emijidius.
Aidha wamemuomba Rais Magufuli, Mkuu wa mkoa pamoja Na maafisa elimu kila wilaya kuonyesha ushiriano ikiwemo kuwawezesha nauli ili waweze kufanikisha kazi hiyo kiurahisi.
"Tunamuomba Rais wetu, mkuu wa mkoa, pamoja Na maafisa elimu wa wilaya kutuunga mkono sambamba Na kutuwezesha nauli ili tuweze kuzifikia shule zilizoko mbali Na Chuo chetu" amesema Emijidius.
Pamoja Na hayo Emijidius amewashauri vijana wenzake walioko kwenye vyuo mbalimbali kujitokeza kufanya shughuli mbalimbali zenye kuleta maendeleo ndani ya jamii Na kuachana Na mambo ambayo hayana faida yoyote ndani ya jamii.
"Nawashauri vijana kutoka vyuo mbalimbali wajitokeze kufanya shughuli mbalimbali zenye kuleta maendeleo ndani ya jamii Na kuachana Na mambo ya kipuuzi" amesema Emijidius.
Comments