MUDAU wa mchezo wa kutunisha misuli Mohamed Ali , ambaye pia ni mmiliki wa
Gym ya mazoezi ya Gymkhana Dar es Salaam amesifia pambano la utunishani wa
misuli liliofanyika ukumbi wa Mayfair jijini Dar es Salaam kati kati ya mwezi Desemba
mwaka jana .
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili Ali alimpongeza mshindi huyo
aliyeibuka na kitita cha Shilingi Milioni 10 na kusema ni moja ya mafanikio
ya kuutangaza mchezo huo kwa siku za hivi sasa.
Washindi wa mwaka jana wa Mashindano ya kutunisha misuli (The Most Musicular Man Tanzania 2014) wa kwanza kutoka kushoto ni msindi wa pili, Omary Lyombe, mshindi wa kwanza Mohamed Nouma (katikati) na mshindi wa tatu, Erick Majura wakionyesha utunishaji misuli wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Gymkana jijini Dar es Salaam wakati huo
Alisema mchezo huo umekuwa ukifanyika nchini kuanzia miaka ya 1990
na kuwa safari katika maisha ya mchezo huo umeonekana ukifanyika katika
hali ya taratibu hivyo onesho hilo limeweza kuonesha hamasa mpya kwa
jamii inayoendelea kufanya mchezo huo.
"Wadau wa mchezo huo kuendelea kushiriki kuna leta hamasa na ushawishi mpya
kwa vijana wapya,kwa wadhamini waliojitokeza kufanikisha shindano hilo mwishoni
mwa mwaka jana wameonesha matumaini mapya katika hali ya upekee kabisa na kuwa
wanasitahili kupongezwa,"alisema Ali.
Ali alisema kuwa kwa zawadi zilizoandaliwa kwa washindi na maandali ya mchezo
huo kweli waandaaji walijitaidi kufanya jihudi nzuri zilizoonesha kuupamba
mchezo huo katika kujenga ushawishi zaidi kwani anaamini kuwa kwa msimu mpya
mwaka huu kutaongezeka mvuto zaidi katika suala la ushiriki wa mchezo huo.
mudau huyo mkubwa katika mchezo huo mwaka 2014 aliandaa shindano lake lililo
itwa ( The Most Musicular Man Tanzania 2014) na ndio mwandaaji wa shindano
lake hilo lililochangia kuleta taswira nyingine katika mchezo huo ambapo moja ya
wadhamini waliojitokeza wakati huo walikuwa ni Torque Tyres, chini ya Mkurugenzi
Mohamed Dewji.
Ambapo kwa mwaka jana Pili Pili Entertainment Company Ltd ya jijini Dar es Salaam
ndio waliokuwa waandaaji na kufanikisha kutoa zawadi kwa washindi ambapo licha ya
kutoa kitita cha Sh.10,000 kwa mshindi huyo pia mshindi aliweza kuondoka na gari.
Comments