Waziri wa maliasili na utalii hapa nchini DR.Hamis Kigwangala(picha na mtandao)
Dar es salaam
Waziri wa maliasili na
utalii hapa nchini DR.Hamis Kigwangala leo amezungumza na wafanyabiashara na wachongaji wa vinyago
katika eneo la Mwenge jijini Dar es salaam, katika ziara yake hii leo, ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye mchango
mkubwa kwenye utalii na kuliingizia taifa kipato.
Baada ya kuwasili
katika eneo hilo na kutembelea baadhi ya
mabanda mbalimbali ya sanaa hiyo, Dk.Kigwangala
amesikiliza changamoto mbalimbali zinazo wakabili wachongaji wa vinyago.
Dk.Kigwangala amewataka
wafanyabiashara hao kumaliza changamoto zao, ili serikali iweze kurahisisha
mipango juu ya wachongaji na wafanyabiasahara wa eneo hilo.
Dk.Kigwangala aliendelea
na ziara yake ambapo pia hii leo amewatembelea wasanii wa sanaa ya uchoraji
manispaa ya kinondoni katika eneo la Morogoro store maarufu tingatinga, na kusema kuwa seriakali kupitia utalii
inataka kila mwananchi kuweza kufaidika na sekta utalii hapa nchini.
Kwa upande wao viongozi
wa Morogoro store maarufu tingatinga wamepongeza hatua ya waziri wa maliasili
na utalii kuithamini kazi yao kwa kuwatembelea na kuwajuza mipango ya serikali.
Awali Waziri Dk.Kigwangala
ametembelea kituo utalii cha kumbukumbu ya hayati mwalimu nyerere kilichopo
magomeni kota jijini hapa nakujionea changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo
hicho, ambacho kilikuwa nyumba ya mwalimu nyerere miaka ya nyuma na kuahidi
kuzitatua changamoto hizo.
Kazi ya sanaa ni kama
kazi nyingine hapa nchini watanzania tuwajali na kuwathamini wasanii wa
uchongaji na uchoraji ili waweze kutimiza malengo yao, na kuondokana na dhana
ya wataii ni watu kutoka nje ya nchi.
Comments