Rais wa Sudan Omar Al Bashir
Sudan imemwagiza Balozi wake nchini Misri kurejea nyumbani mara moja kwa mashauriano zaidi na serikali yake.
Wizara ya Mambo ya nje jijini Khartoum haijatoa maelezo yoyote ni kwanini imefikia maamuzi hayo.
Aidha,haijafahamika wazi ni lini Balozi huyo atasalia nyumbani.
Hatua hii imeishangaza Misri, ambayo kupitia Wizara ya Mambo ya nje imesema inathathmini uamuzi huo kabla ya kuchukua hatua.
Hata hivyo, nchi hizo mbili zimekuwa zikivutana kuhusu mmiliki wa eneo la Halayeb Triangle katika mpaka wa mataifa hayo mawili.
Suala lingine ambalo limekuwa tata kuhusu nchi hizo jirani ni matumizi ya maji ya mto Nile, ambayo yanapitia nchini Sudan kwenda nchini Misri.
Hivi karibuni, Khartoum imekuwa ikiishtumu Cairo kwa kupiga marufuku bidhaa zake hasa za kilimo tangu mwaka uliopita.
Misri imakasirishwa sana na hatua ya Ethiopia kutumia maji ya Mto.Nile kuzalisha umeme.
Comments