Skip to main content

Posts

Showing posts from 2015

BAADA YA KUWATUMBUA WAKWEPA KODI,WAZIRI WA FEDHA ATANGAZA KIAMA KWA HAWA,ATOA KAULI NZITO

      BAADA ya kushughulikia wakwepa kodi ndani ya siku 27 alizokaa Mamlaka ya Mapato (TRA), Waziri mpya wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amehamishia nguvu zake katika sekta ya fedha hasa benki, akizitaka zipunguze riba. Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Dar es Salaam jana, baada ya kuapishwa na Rais John Magufuli, Dk Mpango aliahidi kushughulikia tatizo la riba kubwa, inayotolewa kwenye benki za hapa nchini, jambo linalochangia kushusha idadi ya watu wanaokwenda benki kukopa. “Lazima sekta ya fedha isimamiwe vizuri ili kila mwananchi aweze kukopa, nitahakikisha riba za mikopo zinashuka ili wananchi wajipatie mikopo kwa riba nafuu,” alisema Dk Mpango. Born in Tanganyika to Nyerere Burito (1860–1942), Chief of the Zanaki,Nyerere was known by the Swahilihonorific Mwalimu or 'teacher', his profession prior to politics. He was also referred to as Baba wa Taifa (Father of the Nation).Nyerere received his higher education at Makerere Univer

Homecoming live ndani ya Sinema Zetu ya Azam

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Azam Media itaonesha live uzinduzi wa filamu ya Homecoming utakaofanyika keshokutwa katika Ukumbi wa Mlimani City. Azam kupitia king’amuzi chake itaonesha uzinduzi huo kupitia Chanel yake ya Sinema Zetu ambapo pia watangazaji wake watafanya mahojiano ya moja kwa moja na wageni watakaohudhuria hafla hiyo. Akizungumzia kuhusiana na hatua hiyo ya kuonesha tuko hilo Meneja Masoko wa Azam Mgope Kiwanga alisema kuwa king’amuzi hicho kinatambua nafasi ya filamu katika maendeleo ya sanaa na ndio maana imeamua kuunga mkono uzinduzi huo. Alisema kuwa Azam kupitia chanel yake hiyo wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa wapenzi wa filamu za hapa nyumbani wanaangalia kila kinachoendelea katika tasnia hiyo na ndio wameamua kuwaunganisha moja kwa moja kuona tukio hilo. “Sinema Zetu ni channel ambayo tuliiweka maalum kwa ajili ya filamu za kitanzania na hii filamu ya Homecoming ni zaidi ya filamu kwa kuwa kwanza ina viwango vya uhakika na wanan

Akudo yaanza kuonesha upya wake

 BENDI ya muziki wa dansi ya Akudo Impact 'Vijana wa Masauti' imeanza safari nyingine katika angaza utoaji wa burudani,ambapo meneja wa bendi hiyo Ramadhani Pesambili amesema huo ni moja ya mikakati  kamambe kuongeza vionjo, mvuto na ubora wa bendi hiyo. Akizungumza blog hii katika Bonanza la bendi hiyo la kila siku za Jumapili kwenye ukumbi wa Msasani Beach, Ramadhan alisema tayari katika mipango yakuja na utoaji mpya wa burudani ulionza kufanyika hivi karibuni tumebadilisha uongozi. Alisema Meneja wa bendi hiyo ulimvua madaraka yake aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo awali mwanamuziki Tarsis Masela ambapo mwanamuziki mwingine toka bendi hiyo Zagreb Butamu aliteuliwa na tayari ameonesha kumudu nafasi hiyo. "Zagreb Butamu ameonesha kupendwa zaidi na wanamuziki wenzake naamekuwa na maelewano mazuri na wenzake hivyo anaonekana kumudu kwani kiongozi ni muhimu kukubalika kwanza kwa anaowaongoza,"alisema . Ramadhani alisema kuwa mambo mengi yame

Akudo yaanza kuonesha upya wake

 BENDI ya muziki wa dansi ya Akudo Impact 'Vijana wa Masauti' imeanza safari nyingine katika angaza utoaji wa burudani,ambapo meneja wa bendi hiyo Ramadhani Pesambili amesema huo ni moja ya mikakati  kamambe kuongeza vionjo, mvuto na ubora wa bendi hiyo. Akizungumza blog hii katika Bonanza la bendi hiyo la kila siku za Jumapili kwenye ukumbi wa Msasani Beach, Ramadhan alisema tayari katika mipango yakuja na utoaji mpya wa burudani ulionza kufanyika hivi karibuni tumebadilisha uongozi. Alisema Meneja wa bendi hiyo ulimvua madaraka yake aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo awali mwanamuziki Tarsis Masela ambapo mwanamuziki mwingine toka bendi hiyo Zagreb Butamu aliteuliwa na tayari ameonesha kumudu nafasi hiyo. "Zagreb Butamu ameonesha kupendwa zaidi na wanamuziki wenzake naamekuwa na maelewano mazuri na wenzake hivyo anaonekana kumudu kwani kiongozi ni muhimu kukubalika kwanza kwa anaowaongoza,"alisema . Ramadhani alisema kuwa mambo mengi yame

Uganda kuitisha tena mazungumzo ya Burundi

Uganda imesema itaitisha tena mazungumzo ya upatanishi ya Burundi, kufuatia machafuko yaliyoipeleka nchi hiyo ndogo kwenye kingo za vita na kuulazimu Umoja wa Afrika kujitayarisha kutuma kikosi cha kuwalinda raia. Serikali ya Burundi na pia kundi kubwa zaidi la upinzani wamekaribisha hatua ya kuanzisha tena mazungumzo hayo. Siku ya Ijumaa, (18.12.2015) Umoja wa Afrika ulisema unajiandaa kutuma kikosi cha wanajeshi 5,000 nchini Burundi kuwalinda raia, ukitumia nguvu kwa mara ya kwanza kutuma wanajeshi katika nchi mwanachama dhidi ya matakwa ya nchi hiyo. Hali ya wasiwasi umekuwa ikiongezeka nchini Burundi hasa tangu watu wenye silaha walipovamia kambi za kijeshi katika mji mkuu Bujumbura wiki iliyopita, na kuzusha hofu katika kanda hiyo ambako kumbukumbu za mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 katika nchi jirani ya Rwanda zingalipo. Burundi ilitumbukia katika mgogoro mwezi Aprili baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza mipango ya kuwan

Rais Magufuli amtimua Dkt. Edward Hosea TAKUKURU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dkt. Edward Hoseah kutokana na kutorishwa na namna taasisi hiyo ilivyokua ikitekeleza wajibu wake katika kukabiliana na rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika bandari ya Dar es Salaam. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bwana VALENTINO MLOWOLA kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU. Balozi Sefue amebainisha kuwa, Rais Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa utendaji kazi wa TAKUKURU chini ya Dkt. Edward Hoseah hauwezi kuendana na kazi anayoitaka. “Eneo mojawapo la upotevu mkubwa wa mapato ya serikali ni Bandarini na Katika Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Hivyo Mheshimiwa Rais amesikitishwa na kitendo cha t

Serikali yatoa siku 14 kwa Wageni walioajiriwa nchini bila kuwa na vibali halali

'WANA LAMBALAMBA'AZAM FC YATEKELEZA AGIZO LA DR. MAGUFULI KWA VITENDO

Viongozi wa benchi la ufundi la Azam Academy wakishiriki shughuli za usafi kwenye Zahanati ya Chamazi Kikosi cha Azam FC leo kimetekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Mgufuli alilolitoa majuma machache kabla ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanganyika kwamba, siku ya kuadhimisha Uhuru wa Tanganyika December 9 wananchi wote wafanye usafi kwenye maeneo yanayowazguka ili kuzuia magonjwa mbalimbali yasababishwayo na uchafu. Katika kutekeleza agizo hilo la Rais Magufuli, kikosi cha Azam FC kwa kushirikiana na wananchi leo kimefanya usafi kwenye Zahanati ya Chamazi iliyopo eneo la Chamazi-Mbande, Manispaa ya Temeke kwa kusafisha mazingira yanayoizunguka zahanati hiyo. Wachezaji wakimwaga taka baada ya kusafisha mazingira yanayozunguka eneo la Zahanati ya Chamazi Asilimia kubwa ya wachezaji, makocha na viongozi wengine walikuwa wanatoka katika kikosi B kutokana na kikosi cha kwanza kuwa kwenye maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhid

Hatari

Tupia macho kusoma mambo ya Samuel L Jackson

Samuel L Jackson ni mmoja wa Wamarekani weusi waliofanikiwa sana Hollywood Nyota wa Hollywood Samuel L Jackson atahamia Afrika Kusini iwapo Donald Trump atashinda uchaguzi wa urais Marekani, tovuti ya News 24 imeripoti. Trump, mmoja wa wanaowania tiketi ya kugombea urais Marekani kupitia chama cha Republican, ameshutumiwa vikali baada ya kupendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani. Haijabainika iwapo matamshi ya mwigizaji huyo, yaliyopeperushwa kwenye sehemu ya kipindi cha Jimmy Kimmel Live iliyorekodiwa awali Jumatatu, yalitolewa kabla au baada ya matamshi hayo ya majuzi zaidi kutoka kwa Trump. Trump akemewa kwa kutaka Waislamu wasiingie Marekani Bw Trump, wakati mmoja amewahi kunukuliwa akikosoa kundi linalotetea haki za watu weusi Marekani la Black Lives Matter. BBC

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana azungumza na waandishi

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na waandishi wa habari jana Desemba 8, 2015, katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo) Juzi tarehe 07/12/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilifanya kikao chake cha kawaida mjini Dar es salaam kwa siku moja. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Kamati Kuu pia ilipokea taarifa juu ya utendaji wa Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020. Kwa ujumla na kwa kauli moja Kamati Kuu ya CCM Taifa iliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu na Waziri Mkuu Mhe. Kassim M. Majaliwa kwa kasi nzuri waliyoanza nayo katika

Soma Stori ya Sanamu hii

DBanj alalama kuibiwa idea

Producer wa muziki wa msanii DBanj ‘Deevee’ ametoa malalamiko yake juu ya msanii ambaye ana imani kuwa anawaibia mawazo yao ya muziki. Deevee ametoa malalamiko kuwa rapa Mnigeria Olamide amekuwa akiiba idea za muziki wake na D’banj kila anapoenda kuwatembelea. Deevee aliandika habari hizi za kushtua kwenye kurasa yake ya twitter. Deevee pia amemuomba boss wake D’Banj msamaha kwa kuweka wazi habari hii. With due respect @olamide_YBNL, hav u ran out of ideas? Everytym u come 2 our zones u always gotta steal some idea..I won’t let this fly — #OminiProducer (@IamDeeveeLee) December 4, 2015. I’m vry sry boss @iamdbanj I mean no disrespect but i hv stayd silent 4 too long & I’m ready 2 face d consequences, for dropping the #OminiProducer (@IamDeeveeLee) December 4, 2015. Deevee, anasema Olamide ameiga wazo la wimbo “Shake It” wa DBanj.

NYOTA WA TANZANIA SAMATTA, ULIMWENGU WAMFUATA LIONEL MESSI.

Kikosi cha  TP Mazembe, leo kinakamata pipa kuanza safari ya kwenda nchini Japan. Watanzania wawili, Mbwana Samatta na mshkaji wake, Thomas Ulimwengu watakuwa sehemu ya msafara huo wa mabingwa hao wa Afrika kwenda kucheza michuano ya Kombe la Dunia kwa klabu. Ulimwengu amezungumza kutoka Lubumbashi na kusema: "Tunaondoka kesho (leo), mimi pia nipo vizuri. Kweli niliumia kidogo lakini nimepata matibabu na sasa niko vizuri." Wawili hao wanaendelea kuweka rekodi kwa mara nyingine ya kuwa Watanzania wa kwanza kucheza michuano ya Kombe la Dunia kwa klabu. Mazembe ya DR Congo, inacheza michuano hiyo baada ya kubeba ubingwa wa Afrika kwa kuifundisha kazi USM Alger ya Algeria kwa kuifunga mechi zote mbili za nyumbani na ugenini.

WACHEZAJI AZAM FC KUKATWA MISHAHARA.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, amewachimba mkwara wachezaji wa timu hiyo kuelekea mchezo dhidi ya Simba kwa kuwataka wasizungumze na na mtu yeyote wa nje ya Azam FC kuhusiana na mechi hiyo ambayo presha yake imeshaanza kupanda. Simba na Azam FC zinatarajia kukutana wikiendi hii katika Uwanja wa Taifa huku kukitarajiwa kuwa na upinzani mkali katika mechi hiyo ambayo kila upande utahitaji kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya msimamo wa ligi. Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd, ameeleza kuwa kocha amewataka wachezaji wote kutozungumza na mtu yeyote kuelekea mchezo huo na atakayebainika amezungumza atakatwa mshahara. “Kocha amewakataza wachezaji wote wa Azam kuzungumza kitu kuelekea mchezo wetu dhidi ya Simba na hata mchezo mwingine wowote, jambo hili limeandikwa hata kwenye mikataba yao, yeyote atakayekiuka agizo hili atakatwa mshahara. “Tumejiandaa vyema kuelekea mchezo huo na baada ya kurejea Tanga tutaweka kambi ya pamoja na wachezaji tulio

Kanye West na Kim watangaza jina la mtoto wao wa kiume

Kim na Kanye West wametangaza jina la mtoto wao wa kiume Kim Kardashian ametangaza kwamba yeye na Kanye West wamempa mtoto wao wa kiume jina Saint. Kim alitakiwa kujifungua Saint siku ya Krismasi lakini mtoto huyo amewasili wiki tatu kabla. Kanye hupenda kujiita Yeezus wakati akiimba, na aliachiwa wimbo “I Am God” mwaka 2013.

Wasome nyota wa soka waliobeba tuzo La Liga

Neymar Jr akiwa ameshika tuzo ya mchezaji bora wa La Liga katika mwezi Novemba. Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Neymar Jr 23, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa La Liga wa mwezi Novemba na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Barca kuchukua tuzo hiyo tangu kuanzishwa kwake Septemba 2013. Neymar Jr ambaye ni kinara wa magoli La Liga mpaka sasa, amechukua tuzo hiyo baada ya kufunga magoli matano katika mechi 3 alizocheza katika mwezi huo. Diego Simeone Wakati huohuo kocha wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone, amechukua tuzo ya Kocha bora wa mwezi Novemba katika La Liga baada ya kushinda mechi zote 3 za Ligi hiyo katika huo, hii ni mara ya pili Muargentina huyo anashinda tuzo hiyo.

Nape amwaga pikipiki Mtama

Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akimkabidhi Katibu wa Kata ya Mtua Kilimahewa Ndugu Maliki funguo ya pikipiki kwa niaba ya makatibu kata 20 wa jimbo hilo ambao wote wamewezeshwa usafiri wa pikipiki ili kurahisisha ufanisi wa kazi zao Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye akijaribu moja ya pikipiki kati ya 20 alizowapa makatibu kata ili ziweze kuwasaidia kufanya kazi kwa ufanisi kwenye shughuli zao za kujenga na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi Sehemu ya pikipiki zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye kwa makatibu kata 20 wa jimbo hilo Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akizungumza mbele ya viongozi wa CCM wilaya ya Lindi vijijini ambapo aliwaambia viongozi hao kuwa amejipanga kufanya kazi katika jimbo hilo zenye kuleta tija na kuhakikisha anatekeleza ahadi zote alizozitoa wakati wa kampeni na kuwata makatibu kata waliokabidhiwa pikipiki 20 kuzitumia katika kazi za kujenga na kuimarisha chama. Pic

Manji amwandikia barua Magufuli

Mwenyekiti wa Kampuni ya Quality Group Yusuf Manji Mwenyekiti wa kampuni ya Quality Group, Yusuf Manji amemwandikia barua Rais John Magufuli kumuelezea mchakato wa zabuni aliyoshinda kuendeleza ufukwe wa Coco maarufu kama Coco Beach uliopo Kinondoni. Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo kwa vyombo vya habari jana ilisema Manji aliandika barua hiyo Desemba 5 mwaka huu akimuelezea kiongozi huyo wa nchi usahihi wa mchakato wa zabuni ya kuendeleza eneo hilo akiwa ameambatisha majibu ya pendekezo la mradi huo kuwa lilitakiwa kutekelezwa na kampuni tanzu ya QGL, Q Consult Ltd. Alisema kampuni hiyo ilishinda zabuni kwa kufuata masharti na vigezo vilivyokuwa vimependekezwa na Manispaa ya Kinondoni. Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Manji katika barua hiyo alionekana “kuisemelea” Manispaa hiyo kuwa Januari 20 mwaka huu QCL aliiandika barua yenye kumbukumbu namba QCL/KMC/01/15 ili kusuluhisha kesi hiyo iliyokuwa mahakamani kwa muda mrefu, la

‘King’ Kibadeni aula Kilimanjaro Stars

Abdallah Kibadeni akiwa na kocha wa Taifa Stars Charles Mkwasa (kulia) Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemteua Abdallah Kibadeni kuwa kocha mkuu wa timu wa Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Star’ akisaidiwa na Juma Mgunda kuelekea katika michuano ya CECAFA Chelenji itakayoanza kutimua vumbi Novemba 21 mjii Addis Ababa, Ethiopia. Kilimanjaro Stars inashiriki michuano hiyo mikongwe kabisa barani Afrika, ambapo jumla ya nchi 12 wanachama wamedhibitisha kushiriki michuano hiyo itakayomalizika Disemba 6 mwaka huu. Nchi zingine zinazoshiriki michuano hiyo ni tofati na Tanzania bara ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudani, Sudani Kusini, Uganda na Zanzibar. Kibadeni mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, na timu ya Taifa Tanzania, ni kocha mwenye leseni B, ambapo ameshafundisha vilabu vingi chini kwa mafanikio ikiwemo kuifiksha klabu ya S

Kufuatia Vuguvugu za kisiasa Afande Sele kuacha muziki kushika jembe

Aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Morogoro mjini kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Suleman Msindi alimaarufu kama 'Afande Sele' amefunguka na kusema hawezi kufanya muziki tena, na badala yake atajikita katika shughuli za kilimo. Afande Sele amesema haya katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio na kudai sasa atafanya kilimo pamoja na ufugaji na maamuzi haya yamekuja kutokana na yeye kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu, na ameamua iwe hivyo kwa sababu tayari anaamini amepoteza mashabiki wake wengi ambao walikuwa Ukawa na CCM ambao walikuwa wanaamini katika maono na mashairi yake. “Kwa sasa nimeamua tu kufanya kilimo pamoja ufugaji sitafanya muziki tena sababu nilipoingia kwenye siasa mlango nilioingilia huu wa ACT-Wazalen

OZIL AWEKA REKODI MPYA EPL

Mpika mabao wa Arsenal Mesut Ozil ameweka rekodi mpya katika Ligi Kuu nchini England (EPL) baada ya kutoa pasi za magoli katika michezo sita mfululizo. Mjerumani huyo alitoa pasi ya goli kwa Kieran Gibbs katika mchezo wa jana dhidi ya Tottenham ulioisha kwa sare ya goli 1-1, mchezo uliopigwa kwe ye dimba la Emirates. Ozil ameisaidiz Arsenal kushinda michezo mitano na kutoka sare mchezo mmoja katika michezo sita ya mwisho aliyocheza na kupelekea Arsenal kushika nafasi ya pili nyuma ya Man City wakizidiwa kwa tofauti ya mabao. Ozil amekuwa mchezaji wa kwanza kutoa pasi 10 za magoli katika michezo 11 ya mwanzo ya Ligi Kuu nchini Enlgand.

Ben Pol na Mwana FA wakifanya video Africa Kusini Patoranking naye ndani

Rnb super staa Ben Pol ametimiza ahadiyake ya kwenda Africa Kusini kufanya video ya nyimbo mbili kama alivyo sema awali. Staa huyu pia amekutana na msanii wa dance hall kutoka Nigeria Patoranking na Ben Pol anasema “Alikutana na Patoranking juu kwa juu tu na hawakupata muda wa kuongea mengi ila walibadilishana mawasiliano ” Ben alikutana na Patoranking kwenye show yake ya My Woman mjini Johannesburg Africa Kusini. Ukiacha Ben Pol,Mwana Fa pia naye yupo Africa Kusini akifanya video ambayo hatujui ni wimbo gani na ni muongozaji gani.

Tazama ilikuwa (Live) mkutano wa Magufuli jijini Dar es Salaam

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli anaendelea kufanya mikutano ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. Magufuli amefanya kampeni katika Uwanja wa Biafra wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

NEC yabaini kasoro 300 katika Daftari

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imesema uchakataji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura umekamilika na wamebaini kasoro ndogo ndogo takriban 300 ambazo zimeondolewa. Mkurugenzi wa Daftari na Tehama wa Nec, Dk. Modest Kipilimba, alisema walianza na kasoro 17 zilizobainishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Ukawa walibainisha kasoro hizo katika kituo cha mpigakura cha Ofisi ya Kitongoji Azimio 1, chenye namba 10101010102, kilichopo mtaa wa Mahoma/Makulu, Kata ya Chahwa, jimbo la Dodoma Mjini. Ukawa walibainisha vivuli, mabati, hoteli, watu waliojipiga picha wenyewe, Wazungu, Wachina na vivuli vikiwa vimepewa namba ya mpigakura na majina yasiyoeleweka. “Tumeondoa kasoro nyingi sana na kituo cha Azimio kwa sasa hakuna kasoro yoyote, mbali na kasoro hizo, kasoro nyingi ni za jinsia, kujirudia, jina kutokuonekana,

CHEKI INSHU HII MBEYA CITY WAMKATA HARUNA MOSHI BOBAN

Kiungo mshambuliaji mpya wa Mbeya City, Haruna Moshi ‘Boban’ ameondolewa katika kikosi cha timu hiyo mpaka mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakapoanza mwezi Desemba. Boban alikamilishiwa fedha zake za usajili na City wiki iliyopita na kujiunga na timu hiyo ili kuongeza nguvu baada ya kuwa na mwanzo mbovu msimu huu. Kocha Mkuu wa Mbeya City, Meja Mstaafu, Abdul Mingange,  alisema Boban hajacheza Ligi Kuu kwa muda mrefu na pia amenenepa sana hivyo anahitaji mazoezi maalum mpaka wakati wa mzunguko wa pili ndipo atakuwa fiti. “Boban ni mchezaji mzuri, ana kipaji na uzoefu mkubwa Ligi Kuu, tuna imani kuwa atatusaidia katika mechi zetu lakini siyo kwa sasa kwani amekuwa mzito sana,” alisema Mingange. “Anatakiwa kufanya mazoezi ya ziada, nimempa programu ya kukimbia kuzunguka uwanja mara tano au zaidi kila siku kabla ya mazoezi ya kawaida, anatakiwa kupungua ili aweze kwenda na kasi ya ligi.”Inatoka kwa mudau

Nyota ya Diamond yazidi kung'ara ashinda ‘Best African Act’ ya MTV EMA, kushindana na Priyanka Chopra katika ‘Best Worldwide Act’

Diamond akiwa na tuzo nchini Marekani Msanii Diamond Platnumz kutoka Tanzania ndio mshindi wa kipengele cha ‘Best African Act’ cha Tuzo za MTV Europe kilichokuwa kinashindaniwa na mastaa wengine wa Afrika ikiwemo AKA (South Africa), Yemi Alade (Nigeria), Davido (Nigeria) na DJ Arafat. Diamond ameungana na mshindi wa India Priyanka Chopra kuwania Tuzo ya ‘Best Worldwide Act: Africa/India’. Tuzo alizonyakuwa Diamond Mwaka jana Sauti soul waliibuka washindi wa kipengele cha African Act japo hawakufanikiwa kushinda Tuzo ya ‘World Wide’.