Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemteua Abdallah Kibadeni
kuwa kocha mkuu wa timu wa Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Star’
akisaidiwa na Juma Mgunda kuelekea katika michuano ya CECAFA Chelenji
itakayoanza kutimua vumbi Novemba 21 mjii Addis Ababa, Ethiopia.
Kilimanjaro Stars inashiriki michuano hiyo mikongwe kabisa barani
Afrika, ambapo jumla ya nchi 12 wanachama wamedhibitisha kushiriki
michuano hiyo itakayomalizika Disemba 6 mwaka huu.
Nchi zingine zinazoshiriki michuano hiyo ni tofati na Tanzania bara
ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudani,
Sudani Kusini, Uganda na Zanzibar.
Kibadeni mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, na timu ya Taifa
Tanzania, ni kocha mwenye leseni B, ambapo ameshafundisha vilabu vingi
chini kwa mafanikio ikiwemo kuifiksha klabu ya Simba katika hatua ya
fainali ya kombe la Washindi mwaka 1993.
Kocha Kibadeni ni mkurugenzi wa ufundi wa kituo cha mchezo cha KISA
kilichopo Chanika, amewahi pia kuzifundisha timu za Kagera Sugar, JKT
Ruvu.
Kocha msaidizi wa Kilimanjaro Stars, Juma Mgunda ana leseni B ya CAF,
zamani alikuwa mshambuliaji wa timu ya Coastal Union na timu ya Taifa
Tanzania, pia aliweza cheza soka la kulipwa katika klabu ya Nahd nchini
Oman.
Mgunda amewahi kuifundisha timu ya Coastal Union ya jijini Tanga,
timu ya mkoa wa Tanga, kocha wa kituo cha vijana cha mkoa wa Tanga.
Aidha Mgunda ni mkufunzi wa msaidizi wa mafunzo ya makocha ngazi pevu.
Comments