Mpika mabao wa Arsenal Mesut Ozil ameweka rekodi mpya katika Ligi Kuu
nchini England (EPL) baada ya kutoa pasi za magoli katika michezo sita
mfululizo.
Mjerumani huyo alitoa pasi ya goli kwa Kieran Gibbs katika mchezo wa
jana dhidi ya Tottenham ulioisha kwa sare ya goli 1-1, mchezo uliopigwa
kwe ye dimba la Emirates.
Ozil ameisaidiz Arsenal kushinda michezo mitano na kutoka sare mchezo
mmoja katika michezo sita ya mwisho aliyocheza na kupelekea Arsenal
kushika nafasi ya pili nyuma ya Man City wakizidiwa kwa tofauti ya
mabao.
Ozil amekuwa mchezaji wa kwanza kutoa pasi 10 za magoli katika michezo 11 ya mwanzo ya Ligi Kuu nchini Enlgand.
Comments