Kiungo mshambuliaji mpya wa Mbeya City, Haruna Moshi ‘Boban’
ameondolewa katika kikosi cha timu hiyo mpaka mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara
utakapoanza mwezi Desemba.
Boban alikamilishiwa fedha zake za usajili na City wiki iliyopita na kujiunga na timu hiyo ili kuongeza nguvu baada ya kuwa na mwanzo mbovu msimu huu.
Kocha Mkuu wa Mbeya City, Meja Mstaafu, Abdul Mingange, alisema Boban hajacheza Ligi Kuu kwa muda mrefu na pia amenenepa sana hivyo anahitaji mazoezi maalum mpaka wakati wa mzunguko wa pili ndipo atakuwa fiti.
“Boban ni mchezaji mzuri, ana kipaji na uzoefu mkubwa Ligi Kuu, tuna imani kuwa atatusaidia katika mechi zetu lakini siyo kwa sasa kwani amekuwa mzito sana,” alisema Mingange.
“Anatakiwa kufanya mazoezi ya ziada, nimempa programu ya kukimbia kuzunguka uwanja mara tano au zaidi kila siku kabla ya mazoezi ya kawaida, anatakiwa kupungua ili aweze kwenda na kasi ya ligi.”Inatoka kwa mudau

Comments