.
Taifa Stars imeanza vizuri kampeni ya kuwania kucheza Kombe
la Dunia baada ya kuitwanga Malawi kwa mabao 2-0.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Stars ilipata mabao yake yote mawili katika kipindi cha kwanza.
Bao la kwanza, lilitupiwa kimiani mapema tu na Mbwana
Samatta ambaye alikuwa mwepesi kuiwahi pasi maridadi ya Thomas Ulimwengu na
kufunga kwa ustadi mkubwa.
Ulimwengu, safari hii akipata ‘zawadi’ kutokana na
kumfuatilia kipa wa Malawi aliyeutema mpira wa krosi wa Haji Mwinyi.
Hata hivyo, Malawi walionekana matata zaidi katika kipindi
cha kwanza mwanzo wakitawala dakika zote 15 za mwanzo.
Stars ikageuka na kutawala dakika zote za katikati kabla ya wageni kurejea na kutawala kipindi cha pili mwishoni.
Kipindi Kocha Charles Boniface Mkwasa akiwa anaingoza Stars
kwa mara ya kwanza akiwa Kocha Mkuu mwenye mkataba, aliwatoa Mrisho Ngassa
akamuingiza Salum Telela na Simon Msuva akaingia badala ya Thomas Ulimwengu.
Mchezaji mwingine aliyeingia ni Ibrahim Ajibu na kufufua
nguvu ya ushambuliaji ya Stars.
Hata hivyo, katika kipindi cha pili Stars walitoa nafasi
nyingi zaidi kwa Malawi kushambulia zaidi.
Comments