Nimepokea
kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa NLD na mwenyekiti
mwenza wa UKAWA katika uchaguzi mkuu huu, Mzee Emmanuel Makaidi,
aliyefariki leo katika hospitali ya Nyangao Lindi kwa maradhi ya
shinikizo la damu.
Mzee Makaidi ulikuwa Simba wa mabadiliko. Pamoja na umri wako mkubwa lakini muda wote uliweza kuhimili vishindo vya mahasimu wa mabadiliko. Ulipambana mpaka pumzi yako ya mwisho katika kuleta mabadiliko ya kisiasa ambayo ndiyo kiu ya watanzania.
Mzee Makaidi ulikuwa moja ya nguzo imara katika umoja wetu wa UKAWA, hekima, busara na uaminifu wako ndivyo vilivyoufanya umoja wetu wa UKAWA kuwa tumaini jipya na pekee kwa Watanzania.

Umefariki siku 10 tu kabla ya kwenda kupiga kura. Nawaomba Watanzania
tumuenzi shujaa huyu wa mabadiliko kwa kuwapatia kura wagombea wote wa
UKAWA kuanzia ngazi ya udiwani hadi urais. Mzee Makaidi tunakuahidi
kuendeleza bila kuchoka, kazi uliyoiacha ya kuwaletea watanzania
mabadiliko ili waondokane na umasikini.
MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI AMEEN.
MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI AMEEN.
Comments