Nyota ya Diamond yazidi kung'ara ashinda ‘Best African Act’ ya MTV EMA, kushindana na Priyanka Chopra katika ‘Best Worldwide Act’
Msanii Diamond Platnumz kutoka Tanzania ndio mshindi wa kipengele cha
‘Best African Act’ cha Tuzo za MTV Europe kilichokuwa kinashindaniwa na
mastaa wengine wa Afrika ikiwemo AKA (South Africa), Yemi Alade
(Nigeria), Davido (Nigeria) na DJ Arafat.
Diamond ameungana na mshindi wa India Priyanka Chopra kuwania Tuzo ya ‘Best Worldwide Act: Africa/India’.
Mwaka jana Sauti soul waliibuka washindi wa kipengele cha African Act japo hawakufanikiwa kushinda Tuzo ya ‘World Wide’.
Comments