Mwanariadha aliyeko jela Oscar Pistorius anatarajiwa kuachiwa huru
Jumanne baada ya kutumikia miezi 11 tu ya kifungo cha miaka mitano
gerezani.
Mwanasheria wa mwanariadha huyo anayetumia miguu ya bandia
alifanikiwa kuhoji kwamba Oscar anapaswa kuachiwa huru na kutumikia
kifungo cha nje baada ya kutumikia mwaka mmoja wa kifungo cha miaka
mitano kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013.
Awali, Pistorius alitakiwa kuachiwa huru Agosti, lakini waziri wa
sheria aliingilia kati na kusababisha kuchelewa kabla bodi ya msamaha
kufanya uamuzi.
Hata hivyo, bado anakabiliwa na rufaa ya Mahakama Kuu mwezi ujao,
ambapo kama itafanikiwa, ataongezewa mashtaka ya mauaji na kumfanya
afungwe tena kwa kipindi cha miaka 15.
Comments