Samuel L Jackson ni mmoja wa Wamarekani weusi waliofanikiwa sana Hollywood
Nyota wa
Hollywood Samuel L Jackson atahamia Afrika Kusini iwapo Donald Trump
atashinda uchaguzi wa urais Marekani, tovuti ya News 24 imeripoti.
Trump,
mmoja wa wanaowania tiketi ya kugombea urais Marekani kupitia chama cha
Republican, ameshutumiwa vikali baada ya kupendekeza Waislamu wazuiwe
kuingia Marekani.
Haijabainika
iwapo matamshi ya mwigizaji huyo, yaliyopeperushwa kwenye sehemu ya
kipindi cha Jimmy Kimmel Live iliyorekodiwa awali Jumatatu, yalitolewa
kabla au baada ya matamshi hayo ya majuzi zaidi kutoka kwa Trump.
Trump akemewa kwa kutaka Waislamu wasiingie Marekani
Bw Trump, wakati mmoja amewahi kunukuliwa akikosoa kundi linalotetea haki za watu weusi Marekani la Black Lives Matter.BBC
Comments