BENDI ya muziki wa dansi ya Akudo Impact 'Vijana wa Masauti' imeanza
safari nyingine katika angaza utoaji wa burudani,ambapo meneja wa bendi
hiyo Ramadhani Pesambili amesema huo ni moja ya mikakati kamambe
kuongeza vionjo, mvuto na ubora wa bendi hiyo.
Akizungumza blog hii katika Bonanza la bendi hiyo la kila siku za Jumapili kwenye ukumbi wa Msasani Beach, Ramadhan alisema tayari katika mipango yakuja na utoaji mpya wa burudani ulionza kufanyika hivi karibuni tumebadilisha uongozi.
Alisema Meneja wa bendi hiyo ulimvua madaraka yake aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo awali mwanamuziki Tarsis Masela ambapo mwanamuziki mwingine toka bendi hiyo Zagreb Butamu aliteuliwa na tayari ameonesha kumudu nafasi hiyo.

"Zagreb Butamu ameonesha kupendwa zaidi na wanamuziki wenzake
naamekuwa na maelewano mazuri na wenzake hivyo anaonekana kumudu kwani kiongozi ni muhimu kukubalika kwanza kwa anaowaongoza,"alisema .
Ramadhani alisema kuwa mambo mengi yameisha anza kujenga taswira mpya katika bendi hiyo ambapo alitaja majina ya wanamuziki wapya kuwa ni Shella Mama anayepiga gitaa la solo, Chilayert Bamokina (mwimbaji), Dodo, Lightness, Mery na Christine Ngoi aliyejiunga Akudo akitokea kwa kwa mwanamuziki nyota wa Congo Ferre Gola Bataringe maarufu kama Ferre Chair de Poule au Ferre Gola ambapo wete walikuwa jukwaani katika siku hiyo .
Meneja huyo alisema bendi hiyo inaendelea kutambulisha vibao vipya vitatu viitwavyo'Pinga mauaji ya Albino’, ‘Usikate tamaa’na'Wanawake wanaweza’ambapo tayari vinaonekana kupendwa na mashabiki.
Akudo miaka awali ndio ndio bendi ambayo iloiyomtambulisha mwanamuziki mahiri wa dansi Christian Bella wakati ilipotamba na mtindo wa Pekechapecha kabla ya nyota huyo kuhamia kwenye
bendi nyingine ya Malaika .
Katika mkesha wa kuupokea mwaka mpya bendi hiyo imejipanga
kufanya makamuzi yake kama kawaida katika ukumbi wao wa nyumbani Msasani Beach Dar es Salaam.
Comments