Kikosi cha Azam FC leo kimetekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Mgufuli alilolitoa majuma machache
kabla ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanganyika kwamba, siku ya
kuadhimisha Uhuru wa Tanganyika December 9 wananchi wote wafanye usafi
kwenye maeneo yanayowazguka ili kuzuia magonjwa mbalimbali
yasababishwayo na uchafu.
Katika kutekeleza agizo hilo la Rais Magufuli, kikosi cha Azam FC kwa
kushirikiana na wananchi leo kimefanya usafi kwenye Zahanati ya Chamazi
iliyopo eneo la Chamazi-Mbande, Manispaa ya Temeke kwa kusafisha
mazingira yanayoizunguka zahanati hiyo.
Asilimia kubwa ya wachezaji, makocha na viongozi wengine walikuwa
wanatoka katika kikosi B kutokana na kikosi cha kwanza kuwa kwenye
maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba SC unaotarajiwa kuchezwa
siku ya Jumamosi December 12.
Mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Bi Eduiga Mroso ameushukuru uongozi
wa Azam FC pamoja na wachezaji wote walioshiriki kwenye usafi wa maeneo
yanayoizunguka zahanati hiyo na kuiomba timu hiyo kuendeleza ushirikiano
na ujarani mwema uliopo kati yao.
“Tunaishukuru timu ya Azam FC kuamua kuja kwetu kushirikiana na sisi
kuunga mkono kauli ya Rais wetu Magufuli ya kuadhimisha siku ya Uhuru
kwa kufanya usafi kwenye maeneo yanayotuzunguka. Lakini ushirikiano wetu
usiishie hapa bali uende mbali zaidi kwasababu sisi pia ni majirani na
tunawashukuru sana Azam kwa hilo kwasababu wengeweza kwenda sehemu
nyingine lakini waliamua kuja kwetu”, amsesema Bi Mroso.
Kwa upande wa mtendaji mkuu wa kikosi hicho Saad Kawemba amesema
wameamua kufanya usafi kwenye zahanati hiyo ikiwa ni sehemu ya kudumisha
ushirikiano wao na jamii hasa sehemu zenye uhitaji kama zahanati, shule
na sehemu nyingine nyingi.
Pia akaongeza kuwa, zahanati hiyo ipo eneo la jirani na wao hivyo
hata ikitokea mchezaji au mtu yeyote amepatwa na maradhi atapelekwa
kwenye zahanati hiyo kwa ajili ya matibabu na hicho ndio kitu
kilichowasukuma kushirikiana na wakazi wa eneo la Chamazi kufanya usafi
kwenye zahanati hiyo.
“Sisi kama Azam tumeamua kuja kushiriki shughuli ya usafi hapa
kwasababu kwanza tunataka kudumisha ushirikiano wetu na jamii
inayotuzunguka lakini pia kutekeleza agizo la Rais alilolitoa juu ya
maadhimisho ya siku ya leo kwamba itakuwa ni siku ya kufanya usafi na si
sherehe kubwa ya kitaifa”, amesema Kawemba wakati wa zoezi la usafi
kwenye zahanati ya Chamazi.
“Lakini hawa ni majirani zetu, ikitokea mchezaji au kiongozi wa Azam
FC akapatwa na maradhi ataletwa hapa, kwahiyo tukaona ni vyema tuje
kushirikiana na majirani zetu kufanya usafi kwenye eneo la hii zahanati.
Mh. Dr. Magufuli alipiga marufuku kufanyika sherehe kubwa za
maadhidimisho ya siku ya Uhuru ambazo zimekuwa zikigharimu pesa nyingi
na badala yake akaagiza pesa hizo zifanye kazi nyingine za maendeleo ya
jamii na siku hiyo wananchi wote wafanye usafi kwenye maeneo
yanayowanunguka.
Comments