Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart
Hall, amewachimba mkwara wachezaji wa timu hiyo kuelekea mchezo dhidi ya Simba
kwa kuwataka wasizungumze na na mtu yeyote wa nje ya Azam FC kuhusiana na mechi
hiyo ambayo presha yake imeshaanza kupanda.
Simba na Azam FC zinatarajia
kukutana wikiendi hii katika Uwanja wa Taifa huku kukitarajiwa kuwa na upinzani
mkali katika mechi hiyo ambayo kila upande utahitaji kushinda ili kujiweka
katika nafasi nzuri zaidi ya msimamo wa ligi.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd,
ameeleza kuwa kocha amewataka wachezaji wote kutozungumza na mtu yeyote
kuelekea mchezo huo na atakayebainika amezungumza atakatwa mshahara.
“Kocha amewakataza wachezaji
wote wa Azam kuzungumza kitu kuelekea mchezo wetu dhidi ya Simba na hata mchezo
mwingine wowote, jambo hili limeandikwa hata kwenye mikataba yao, yeyote
atakayekiuka agizo hili atakatwa mshahara.
“Tumejiandaa vyema kuelekea
mchezo huo na baada ya kurejea Tanga tutaweka kambi ya pamoja na wachezaji
tuliowaacha kwa ajili ya mazoezi ya pamoja ya kuivaa Simba kwani lengo letu ni
kuhakikisha tunashinda mchezo huo.
“Wachezaji wetu wote wa kimataifa wamesharejea tayari kwa
ajili ya mchezo huo akiwemo Wawa, Tchetche na Bolou,” alisema Idd.Inatoka kwa mdau.
Comments