Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Azam Media itaonesha live uzinduzi wa
filamu ya Homecoming utakaofanyika keshokutwa katika Ukumbi wa Mlimani City.
Azam kupitia king’amuzi chake itaonesha uzinduzi huo
kupitia Chanel yake ya Sinema Zetu ambapo pia watangazaji wake watafanya mahojiano
ya moja kwa moja na wageni watakaohudhuria hafla hiyo.
Akizungumzia kuhusiana na hatua hiyo ya kuonesha
tuko hilo Meneja Masoko wa Azam Mgope Kiwanga alisema kuwa king’amuzi hicho
kinatambua nafasi ya filamu katika maendeleo ya sanaa na ndio maana imeamua
kuunga mkono uzinduzi huo.
Alisema kuwa Azam kupitia chanel yake hiyo wamekuwa
mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa wapenzi wa filamu za hapa nyumbani wanaangalia
kila kinachoendelea katika tasnia hiyo na ndio wameamua kuwaunganisha moja kwa
moja kuona tukio hilo.
“Sinema Zetu ni channel ambayo tuliiweka maalum kwa
ajili ya filamu za kitanzania na hii filamu ya Homecoming ni zaidi ya filamu
kwa kuwa kwanza ina viwango vya uhakika na wananchi wanatakiwa kuoneshwa kila
kitu kuhusiana na filamu hiyo” alisema Kiwanga.
Seko Shamte Producer
Akizungumzia
kuhusiana na filamu hiyo mwongozaji wa Homecoming ambae pia ni Mkurugenzi wa
Alkamist Media, Seko Shamte alisema kuwa filamu hiyo itaanza kuoneshwa rasmi
kwa kiingilio Januari 29 mwakani lakini Desemba 29 mwaka huu ni ndio
inazinduliwa.
Alisema kuwa ni filamu ambayo ina mahudhui
yanayozungumzia masuala ya rushwa kitu ambacho ni kero kubwa kwa wananchi na
jamii nzima kwa ujumla.
Alisema kuwa kutokana na ujumbe wake na namna
ilivyoandaliwa imewavutia wengi ikiwamo kampuni ya Azam Media ambayo kupitia
king’amuzi chake cha Azam kimeamua kuuonesha live uzinduzi kwenye channel ya
Sinema Zetu.
“Ninapongeza Azam kwa moyo wao kwanza wametutangaza
sana wasanii wamefanya mahojiano katika Luninga yao na kisha wataonesha Live
uzinduzi hii ni ishara kuwa tutakuwa nao katika kazi nyingi tu na kwa niaba ya
Alkamist Media tunaahidi kuendelea kuzalisha kazi zenye ubora unaotakiwa”
alisema Seko.
Mwigizaji Mkuu katika filamu hiyo Daniel Kijo
aliwataka wananchi kuiunga mkono filamu hiyo pindi itakapoingia sokoni na
kuoneshwa kwenye majumba ya sinema.
Comments