Klabu ya Yanga imeyaaga mashindano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kukubali kufungwa jumla ya mabao 5-4 kwa njia ya mikwaju ya penati kutoka kwa URA katika hatua ya nusu fainali. Wakusanya mapato ahawa wa Uganda ndiyo waliyoitoa Simba SC kwa bao 1-0 katika hatua ya nusu fainali hivyo kuifanya timu hii kuwafunga hasimu hawa wawili na kuwatoa katika shindano moja.
Mchezo huo iliyokuwa na ushindani mkubwa huku Yanga SC ikionekana kutawala zaidi mpaka dakika 90 zinamalizika mabao yalikuwa 0-0.
Katika hatua ya mikwaju ya penati Yanga SC ilipata mikwaju yake minne kupitia kwa, Tshishimbi, Hassan Hamisi Kessi, Raphael Daudi, Gadiel Michae huku ikikosa moja kupitia kwa mchezaji Obrey Chirwa na kudakwa na mlinda lango wa URA. Mwaka 2016 timu hii iliitoa Yanga kwa njia ya mikwaju ya penati katika hatua kama hii ya nusu fainali na kufanikiwa kutinga fainali.
Mchezo mwingine wa nusu fainali utaikutanisha Azam FC dhidi ya Singida United majira ya saa mbili na robo usiku na fainali inatarajiwa kuchezwa tarehe 13 ya siku ya Jumamosi.
Comments