Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita .
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman
Kapufi akielezea mikakati ya wilaya ya kuhakikisha wanapamba zaidi na
vitendo ambavyo vimeendelea kufanywa na wavuvi ambao awana mapenzi mema
na samaki waliomo kwenye ziwa viktoria wakati wa zoezi la uteketezaji wa
zana haramu.
Wananchi wa Kata ya Nkome wakiwa kwenye
mkutano ambao ulikuwa na lengo la kuelezea hali ya uvuvi haramu ilivyo
kwenye kata ya Nkome na namna ambavyo oparesheni imeweza kufanyika
kwenye maeneo hayo.
Kiongozi wa kikosi maalumu
kinachoendesha oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu ziwa victoria
Gabriel Mageni akielezea namna ambavyo wameweza kuendesha zoezi hilo
ndani ya siku kumi na mbili.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert
Luhumbi akisisita kwa wale ambao ni watumishi na viongozi kuacha
kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu .
Na Joel Maduka,Geita.
Serikali Mkoani Geita Imeteketeza zana
haramu zenye thamani ya shilingi milioni therathini na tatu zikiwemo
Nyavu za makila zilizounganishwa 2,393,makokolo ya sangara 32,timba 142
makokoro ya dagaa 7 na dududu 11.
Hatua hiyo imetokana na oparesheni ya
Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea kwenye maeneo ya
ziwa viktoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi huo ndani ya ziwa hilo
pamoja na kuondoa mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia
,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya
yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.
Zoezi hili la uteketezaji zana hizo
limefanyika kwenye Kata ya Nkome ,ambapo kiongozi wa oparesheni hiyo
Gabriel Mageni ,amemweleza mkuu wa mkoa huo kwamba kuna baadhi ya
wafanyakazi wa hifadhi ya Rubondo wamekuwa wakihusika na uvuvi haramu
kwa kuwaruhusu wavuvi kuingia kwenye hifadhi na wengine kuficha zana zao
ndani ya hifadhi na kwamba wamekuwa wakilipwa fedha wafanyakazi hao
maarufu kwa jina la "KIFUNDA"
Kufuatia malalamiko hayo mtandao huu
umetafuta kwa njia ya simu afisa mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete
alisema kuwa wao kama watu ambao wanamamlaka ya hifadhi za taifa na
kwamba kwa mujibu wa kanuni na taratibu za sheria askari wao hawapaswi
kushiriki kwenye vitendo vya ujangili na kwamba taratibu za kiuchunguzi
zikifanyika na wakabaini kuna watumishi wanajihusisha na vitendo hivyo
hatua za kisheria na za kinidhamu zitachukuliwa na hawawezi kuwakingia
kifua.
Aidha Mageni aliongeza kuwa katika
operesheni hiyo ambayo ina siku kumi na mbili baadhi ya mambo ambayo
wameyabaini ni pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa
wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni
wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na
kusababisha serikali kukosa mapato.
Mkuu wa Mkoa huo,Mhandisi Robert
Luhumbi,amewataadhalisha watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu
na kwamba endapo kuna mtu hakibainika na kitendo hicho serikali
itahakikisha inamchukulia hatua na kwamba kupitia oparesheni hiyo
hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo.
Nyawalwa Wange ni moja kati ya watu
ambao wanajishughulisha na kazi ya uvuvi alisema agizo la Mkuu wa Mkoa
ni la kuungwa mkono kutokana na kwamba uvuvi haramu umeendelea kuharibu
kwa kiasi kikubwa samaki ambao wapo ndani ya ziwa viktoria na kwamba
serikali iendelee kuwabaini wale wote ambao wanaendelea kufanya shughuli
za uvuvi kinyume na sheria.
Katika oparesheni hiyo jumla ya fedha
ambazo zimekusanywa ni zaidi ya milion, 111 fedha zinazotokana na faini
,malipo ya mrahaba pamoja na mauzo ya samaki.
Comments