Richard Kayombo mkurugenzi wa (TRA) Elimu kwa walipakodi
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema , imevunja rekodi ya makusanyo katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha 2017/2018 Julai hadi Desemba 2017 kwa kukusanya sh.trilioni 7.87
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu wa kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo, amesema makusanyo hayo ni makubwa ukilinganisha na kipindi kama hicho kilichopita.
“Katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha 2017/2018 yaani kuanzia Julai hadi Desemba 2017, TRA imekusanya jumla ya sh.trilioni 7.87 ikilinganishwa na sh.trilioni 7.27 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha 2016/2017 ambacho ni sawa na ukuaji wa asilimia 8.45,” amesema Kayombo.
Ameongeza, katika mwezi wa Desemba 2017 pekee, TRA imekusanya sh.trilioni 1.66 ikilinganishwa na makusanyo ya Desemba 2016 ambapo ilikusanya sh.trilioni 1.41 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 17.65.
Comments