Mamlaka ya Usimamizi wa Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) wamekutana na Chama cha Wamiliki wa Mabasi yanayo enda Mkoani (TABOA) kujadili kanuni mpya za leseni za usafirishaji na marekebisho ya baadhi ya kanuni.
Aidha Kahatano amesema kuwa lengo ni utekelezaji wa kanuni utakapo anza kila mtu awe anajua wajibu wake, kuanzia wamiliki mabasi,abiria na madereva ili kuepukana na ajali zisizokuwa za lazima.
kwa upande wa wadau wa SUMATRA walitoa maoni yao kupitia mjumbe
wa halmashauri Kuu ya TABOA Mwesingwa Kazaula wakiomba mamlaka hiyo kupunguza kiasi cha faini kilichopangwa.
Comments