Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan leo Alasiri amehutubia Bunge la nchi hiyo kwa mara ya kwanza juu ya kifo cha Mwandishi wa Habari Jamal Khashoggi aliyeuawa ndani ya Ubalozi wa Saudi Arabia Mjini Instabul mnamo Oktoba 02, 2018.
Erdogan amesema kuwa kifo cha mwandishi huyo kilipangwa na Maafisa wa Saudi Arabia nchini Uturuki na sio kuwa kilitokea kwa bahati mbaya kama serikali ya nchi hiyo ilivyoripoti awali.
Akihutubia kwa hudhuni, Erdogan amesema kuwa siku moja kabla ya kifo cha Khashoggi, maafisa usalama 15 wa Saudi Arabia walijipanga makundi matatu Mjini Instabul ambapo watu 9 waliweka kambi katika msitu wa Belgrad uliopo kilometa 55 kusini mwa Instabul.
Erdogan amesema masaa machache kabla ya Khashoggi kuingia kwenye Ofisi za ubalozi huo kamera za usalama zilizimwa.
“Tumeshawambia kuwa tutaweka ukweli wote hadharani, hatuwezi kunyamaza juu ya tukio hili. Tunaahidi kuchukua hatua zote muhimu hadi kuhahakisha kuwa haki imetendeka,“amesema Erdogan.
Siku ya tukio la kupotea kwa Mwandishi huyo katika Ofisi hizo, Mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman alikaririwa akisema kuwa Khashoggi alitoka akiwa hai kwenye jengo hilo.
Baadae Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Adel al-Jubeir akathibitisha taarifa za kifo cha mwandishi huyo katika Ubalozi wa Saudi Arabia huku akieleza kuwa Khashoggi alileta vurugu kwenye Ofisi hizo.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu leo akiongea mbele ya Waandishi wa Habari naye amesema kuwa Khashoggi kifo chake kilipangwa.
Mpaka sasa mwili Khashoggi bado haujapatikana licha ya Saudi Arabia kukiri mwandishi huyo kuuawa mnamo Oktoba 2 mwaka huu.
Comments