IGP Siamon Sirro ametoaufafanuzi juu ya tukio la kutekwa kwa mfanya biashara Mo ambako mfanyabiashara huyo alipatikana maeneo ya Gymkana jijini Dar Es Salaam. Kupatikana kwa Mo Dewij kumeleta ahueni kwa familia pamoja na wanachi wa Dar Es Salaam kwani imepita sasa takribani wiki moja sasa tangu Mo atekwe na watu wasiojulikana.
Ikumbukwe kwamba jana IGP Sirro alizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio hilo na kufanikiwa kuonyesha picha ya gari iliyotumika kumteka Mo na kwenye picha hiyo namba za gari hilo zilionyesha ni za nchi jirani ya Msumbiji,huku IGP Sirro akisisitiza Polisi bado wanaendelea na uchunguzi. Baada ya kauli hiyo ya Sirro pamoja na kuonyesha picha ya gari hilo ndipo leo gari hilo lilipopatikana maeneo hayo ya Gymkana huku likikutwa na Silaha kali ya kivita AK 47 ikiwa na risasi 19 lakini pia gari hiyo ikiegeshwa pembeni mwa barabara. https://www.youtube.com/watch?v=G8HHcnvQJgE Wakati anaongea na waandishi wa habari IGP Sirro amesisitiza wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwani upelelezi bado unaendelea huku akiwataka wawe na imani na Jeshi la polisi kwani linafanya kazi ipasavyo. Mbali na hilo IGP amewapa onyo kali wale wanaolazimisha uadui na jeshi la polisi na kuuliza “Wanatumwa na nani ? By Ally Juma.
Comments