Dkt. Regnald Mengi kuptia IPP Touchmate Ltd amewekeza bilioni II.5 kuzalisha bidhaa mbalimbali za Kielektroniki.
Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania Dkt. Regnald Mengi ametangaza ujio wa Kampuni Mpya ya IPP Touchmate Ltd ambapo amewekeza bilioni II.5 kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbalimbali za Kielektroniki.
Kampuni hiyo itakuwa ya kwanza Tanzania kuanza kuzalisha bidhaa za Kielektroniki ikiwemo simu za mikononi, simu janja (Smartphones), Computers, Ipads, music bluetooth speakers, headphones pamoja na earphones.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Dkt. Mengi, amesema kuwa lengo kuanzisha kampuni hiyo kuendelea kukuza uchumi wa viwanda pamoja kuzalisha ajira hasa kwa watu wenye ulemavu.
Amesema kuwa kiwanda hicho kinatarajia kutoa ajira rasmi na zisizo rasmi 2,000 jambo ambalo litapunguza changamoto ya kukosefu wa ajira kwa serikali.
"Kampuni hii itatoa kipaombele katika kuajiri wenye ulemavu, wenye sifa stahiki" amesema Dkt. Mengi.
Meneja wa IPP Touchmate Ltd Victor Tesha, amesema kuwa kiwanda hicho kitakuwa maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo kitakuwa kinazalisha bidhaa zenye ubora kwa gharama nafuu.
Tesha amesema kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kuanza kufanya kazi baada miezi mitatu ambapo kwa siku itazalisha simu I,200.
Ameeleza kuwa kiwanda kitatengeneza simu bora ambazo zitakuwa zinakaa na charge kwa zaidi ya wiki moja zikiwa ni maalumu kwa mazingira yenye matatizo ya umeme hasa vijijini.
"Simu zetu zitatumika kama power Bank kucharge simu zingine" amesema Tesha.
Comments