Skip to main content

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekataa kuzindua stendi kuu mpya ya Mailmoja Kibaha

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekataa kuzindua stendi kuu mpya ya Mailmoja Kibaha mkoani Pwani, akiwa katika ziara yake mkoani humo. 

Hatua hiyo ameifikia kutokana na kupata wasiwasi wa utekelezaji wa mradi kuwa na baadhi ya mapungufu ambapo amedai baada ya kufanya uchunguzi wiki mbili ama tatu zijazo atakwenda kuuzindua. Akizungumza katika stand hiyo, Samia alieleza, kuna minong’ono wameisikia kuhusu mradi huo hivyo ni jukumu lake kuibeba na atakapo jiridhisha atarudi kwa mara nyingine . 

Hata hivyo, alisema atakutana na mkuu wa wilaya, mkurugenzi na mkuu wa mkoa kuzungumzia suala hilo. “Msishtuke kwa hili ni kawaida kwa kuchukua hatua za aina hii ili kujiridhisha kwa maslahi ya halmashauri, mkoa na watumiaji kijumla “Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sikivu na kusikia malalamiko ya wananchi, tumepata malalamiko kidogo kuhusu stand hii, serikali ni ya uwazi na ukweli hivyo sitofungua stendi “alisisitiza Samia. 

Samia alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Jennifer Omolo na mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama na wahusika waliohusika kufanikisha mradi huo. Nae waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa -TAMISEMI ,Selemani Jafo alisema yeye kama waziri wapo wataalamu wanaohakiki lakini ameridhishwa na kazi hiyo . 

“Kwani kila kazi ina changamoto za kibinadamu, hasi na chanya, lakini wamejitahidi “alisema Jafo. Jafo alieleza, mradi huo umepata msaada wa mkopo nafuu kutoka bank ya Dunia ambao wamepata fedha za kimarekani dollar milioni 255 .# Alielezea , wanagusa miji 18 na wanachokifanya wanagusa stendi tisa, barabara za miji kwa kiwango cha lami na madaraja makubwa ya kisasa. 

Wakitoa kero ya stand hiyo, madereva pikipiki walidai eneo lililotengwa kwa ajili yao halina sehemu ya kujikinga hivyo kusababisha usumbufu wakati wa mvua na jua. Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Jennifer Omolo alisema katika stendi ndogo ya awali walikuwa wakikusanya ushuru sh. 950.000 kwa siku ambapo sasa wanakusanya sh. milioni 1.6 .Alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 2.9 na walishamlipa mkandarasi bilioni 2.7 ,stendi hiyo itakuwa na mabanda kumi ya kukatia tiketi, mawakala 40 ,eneo la tax, na wafanyabiashara ndogondogo wanaojiingizia kipato kwa kuuza biashara zao wapo 100 . 

Samia akiwa katika ziara yake Kibaha vijijini na mjini pia alipata fursa ya kutembelea mradi wa reli ya kisasa ya standard gauge kujionea namna unavyoendelea.
6
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji Mhandisi Farid M. Abdallah wakati akikagua shughuli za ujanzi wa Reli ya Kisasa “Standard Gauge” katika kijiji cha Soga wilyani Kibaha mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
3
5
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua stendi mpya ya mabasi Kibaha . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
2

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was

HAYA NI MAKAO MAKUU YA MTANDAO WA Tigo TANZANIA DAR ES SALAAM

MAHALA yalipo ni Lugoda Street Gerezani Industrial Area , kwa sasa mdandao huu umefanya makubwa , kuna Tigo Bwerere Uilisha cheki hiyoooooo watu full kujiachia wana chonga tuu kwenye vyao vilonga.