Vodacom Foundation watoa msaada kwa wanafunzi wasioona shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom wakitoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kujisomea kwa wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo jijini Dar es Salaam.
MWAMBA WA HABARI.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, kupitia mpango wake wa pamoja na vodacom wametoa msaada wa vifaa vya kusomea kwa wanafunzi zaidi ya I50 wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo jijini Dar es Salaam.
Msaada huo wametoa kwa ajili kuonyesha ushirikiano na kupatikana kwa elimu bora kwa watu wote kutokana ni moja kati ya nguzo kuu za Asasi ya Vodacom Tanzania Foundation.
Msaada huo ni Mashine kumi
na karatasi maalum za kuchapisha maandishi ya nukta (Maandishi maalum kwa wasioona), viti, faili za plastiki (maalum kwa ajili ya wasioona).
Akizungumza katika hafla fupi ya kutoa vifaa ya kujifuzia Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Dar es Salaam na Pwani George Lugata, amesema kuwa elimu ni haki ya msingi pia n kipengele katika kufikia malengo endelevu.
Kamishna Msaidizi watu wenye ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu, Beatrice Fungamo (Kushoto) akipokea moja ya mashine maalum za kuandikia maandishi ya nukta nundu (Braille) zilizotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC.
Lugata amesema kuwa wanatambua mchango na muhimu wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko katika kuwa kuwafundisha watoto ili wapate elimu bora inayoendana na mahitaji kwa sasa.
Amesema kuwa Asasi ya Vodacom Tanzania Foundation imekuwa ikitumiwa
nawafanya kazi wa Vodacom kurejesha fadhila kwa jamii ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika mazingira rafiki.
“Tuna shauku ya kuisaidia jamii yetu, na huu ni utaratibu wetu kwa miaka zaidi ya 12 kupitia Vodacom Tanzania Foundation tumekuwa tukiisaidia jamii” amesema Lugata.
Amesema kuwa huu ni mwendelezo wa kusaidia jamii, kwani ni nmara ya pili kwa Vodacom kutoa msaada katika shule hiyo, kwani awali walitoa milioni I2 katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko kwa ajili ya kujenga mabweni na vyoo kwa ajili ya wanafunzi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Stella Ikupa Alex, ameishukuru Kampuni ya Vodacom kwa msaada kutokana umepunguza changamoto katika sekta ya elimu.
Comments