KINDA wa Timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys, Ally Hamis Ng'anzi anayecheza nafasi ya kiungo nyota yake imewaka baada ya kupata timu barani Ulaya katika klabu ya MFK Vyskov inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Jamhuri ya Czech.
Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United, Festo Sanga ambayo kinda huyo anaichezea amesema kuwa Ng'anzi amepata nafasi hiyo ya kucheza katika nchi ambayo anatoka mchezaji bora wa Ulaya mwaka 2003, Pavel Nedved ikiwa ni jitihada za klabu hiyo kutafutia wachezaji wake fursa za kucheza nje ya nchi.
Ng'anzi anatarajia kusafiri usiku wa leo kuelekea nchini humo kwa ajili ya kuanza maisha yake mapya ya soka.
" Kwa niaba ya uongozi wa Singida nimtakie kila la heri mchezaji wetu huyu katika safari yake ya soka ambayo anaenda kuianza nchini Czech, hii ni nchi kubwa imetoa wachezaji wakubwa sana akina Nedved, Petr Cech na hata Thomas Rosisky, nidhamu na kujituma pekee ndipo kutampa mafanikio zaidi," amesema Sanga.
Kupata nafasi kwa Ng'anzi kunamfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wa kitanzania wanaocheza barani Ulaya ambapo pia anakipiga nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta katika klabu ya Genk. Wengine ni Rashird Chilunda na Farid Mussa wanaocheza Teneriffe ya nchini Hispania.

- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments