Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) Joyce Msuya akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira January Makamba wakiangalia maonyesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali walizotengeneza kutokana na fursa katika sekta ya mazingira leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Watanzania wametakiwa kutumia njia za kibunifu katika kutumia fursa za uchumi zinazotoka kwenye hifadhi wa mazingira.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye maonyesho ya mjadala kuhusu fursa za uchumi katika mazingira, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) Joyce Msuya, amesema kuwa majukumu yao kutoa ushauri na kusaidia kutatua changamoto za mazingira.
Msuya ambaye ni mgeni rasmi katika mjadala huo, amesema kuwa ili kufika malengo wakati mwengine inapaswa kubadilisha wataalamu jambo ambalo litasaidia kuboresha utendaji katika kupata fursa za kiuchumi kupitia changamoto za mazingira.
"Tumekuwa tukitoa masaada katika kufanikisha usafi wa mazingira lakini tuendelee kuhamasisha uwekezaji katika mazingira" amesema Msuya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira January Makamba , amesema kuwa changamoto za mazingira zinapaswa kutumiwa kama fursa za kujiingizia kipato.
Mhe. Makamba amesema kuwa changamoto za mazingira unaweza kuzitumia kutengeneza fursa za kiuchumi.
"Takataka unaweza ukazalisha nishati ya umeme, mkaa jambao ambalo ni rafiki katika kutatua changamoto za uharibifu wa mazingira pamoja na kujiingizia kipato" amesema Mhe. Makamba.
Amesema kuwa serikali inaendelea kutatua vikwanzo kwa wajasiriamali ambao wamewekeza kupitia mazingira ili kuhakikisha wanakuwa katika mazingira rafiki.
Hata hivyo Mhe. Makamba amesema kuwa bado wanaendelea kutumia mbinu mbalimbali za kuhakikisha watanzania wanapata fursa za kiuchumi ambazo zinaondoa kero ya uchafuzi wa mazingira.
"Bado tuaendelea na mipango ya kuzuia mifuko ya plastic, kwa sasa tumesitisha kutoa vibali kwa kiwanda kinachotaka kuzalisha mifuko hiyo hapa nchini kutokana imeonekana inachafua mazingira" amesema Mhe. Makamba.
Mhe. Makamba amebainisha kuwa serikali ipo katika mipango ya kuwakutanisha wajasiriamali na taasisi za serikali ili ziweze kutumia mkaa mbadala katika matumizi yao.
"Tutaendelea kutengeneza maarifa na shirika la mazingira duniani (UNEP) ili kufika malengo husika" amesema Mhe. Makamba.
Kwa upande wao wadau wa mazingira wamesema kuwa ili kufika malengo serikali inapaswa kutoa ushirikiano kwa wajasiriamali wadago ambao tayari wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya mazingira.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps