Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mwanzilishi na Rais wa Foundation Pour l¨ Enfrance Mama Anne Aymone Giscard d’ Estaing na Mke wa Rais Mstaafu wa Ufaransa Bwana Valery Giscard d’ Estaing, wakati Mama Salma alipotembelea makao makuu ya taasisi hiyo jijini Paris Ufaransa tarehe 22:1:2013: Mama Salma yupo nchini Ufaransa akifuatana na Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini humo:
Rais wa AMREF France Bwana Nicolas Merindol akimkaribisha Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete kwenye makao makuu ya shirika hilo jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 22, 1, 2013 na baadaye viongozi hao walifanya mazungumzo juu ya ushirikiano zaidi wa taasisi hizo katika masuala ya afya na elimu:
Na: Anna Nkinda – Paris
Ushirikiano wa pamoja baina ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na wadau wa maendeleo nchini umeiwezesha taasisi hiyo kuwasaidia na kuwainua wanawake kiuchumi ambao wameweza kujishughulisha na kazi za ujasiriamali na
hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
Pia
Taasisi hiyo imeweza kutoa ufadhili wa masomo kwa watoto yatima na
wanaoishi katika mazingira hatarishi jambo ambalo limewafanya watoto hao
wapate elimu sawa watoto wengine wenye wazazi na kuimarisha afya za
mama wajawazito na watoto
Hayo
yamesemwa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipotembelea
Taasisi inayoshughulika na masuala ya watoto (France Parrainages)
kiliyopo mjini Paris ambacho kinafanya kazi na Kituo cha Ufaransa cha
kuwaangalia watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Partage Tanzania
inayohudumia watoto yatima katika mkoa wa Kagera.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa WAMA alisema kuwa Taasisi hiyo
imeweza kujenga shule ya Sekondari ya WAMA – NAKAYAMA iliyopo Rufiji
Mkoani Pwani ambayo ina wanafunzi 247 ambao ni watoto yatima na
matarajio ya baadaye ni kuwa na wanafunzi 780.
“Katika
mkoa wa Lindi tumejenga mabweni ya wanafunzi wa sekondari wa kike,
tunagharamia masomo ya Sekondari kwa wanafunzi 250 na wanafunzi 16 wa
elimu ya juu kutoka mikoa yote nchini”, alisema Mama Kikwete.
Aliendelea
kusema kuwa Taasisi hiyo imeweza kuwasaidia wanawake kiuchumi na
kuwafanya waweze kuongeza kipato cha familia zao, kutoa elimu ya
ujasiriamali kwa vikundi vidogo vidogo ambavyo vinaweza kutengeneza
bidhaa za kusindika za vyakula na kuziuza.
Kwa
upande wake Charline Flauge’re ambaye ni msimamizi wa Programu za Kituo
cha Ufaransa cha kuwaangalia watoto upande wa Afrika alisema kuwa
Taasisi ya Partage Tanzania ambayo inahudumiwa na kituo hicho inafanya
kazi nchini katika mkoa wa Kagera ambayo ni moja ya nchi tatu muhimu
kutokana na idadi ya watoto wanaowahudumia kufikia 10000.
Alisema
kuwa watoto hao yatima wanaishi vijijini na familia zao
zinajishughulisha na kazi za ukulima mdogo wa kahawa na migomba wao
wanatoa ufadhili ambao unawasaidia waweze kuishi na familia zao na
kupata upendo wa ndugu bila ya kuishi katika vituo vya kulelea watoto
yatima
Flauge’re
alisema, “Tunashukuru kwa kuwahudumia watoto hawa ambao wameweza kukua
wenyewe ndani ya familia zao za mama, kaka au dada, ufadhili huu
umeweza kumsaidia mzazi aliyebaki hai, bibi na babu zao kuwaangalia na
hivyo kukua katika afya njema na mazingira yao waliyozaliwa
Alimalizia
kwa kusema kuwa ufadhili huo hautoi fedha na vitu peke yake bali pia
unajenga mahusiano baina ya watoto na wafadhili wao ambao wanaishi
nchini Ufaransa kwani watoto wanawaandikia wafadhili barua na
kuwasiliana nao na wakati mwingine wanakuja kuwasalimiana nchini
Tanzania na hivyo kujifunza mila na desturi za pande zote mbili.
Taasisi
ya WAMA ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa na malengo ya kutoa ufadhili wa
masomo kwa watoto wa kike ambao hawakupata nafasi ya kusoma, kuimarisha
afya ya mama wajawazito na watoto, kuwainua wanawake kiuchumi na
kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi.Source Mjengwa.
Comments