POLOSI DAR YAWASHIKILIA ASKARI WATANO KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UPOTEVU WA TSHS.150M.ZILIZOPORWA ENEO LA KARIAKOO
Jeshi
la polisi Kanda Maalum Dar es Salaam inawashikilia askari polisi watano
kwa tuhuma za upotevu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 150 mara
baada ya tukio la uporaji lililofanyika eneo la Kariakoo mnamo tarehe
14/12/2012.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa
Polisi, Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam Suleiman Kova (pichani)
amesema baada ya tukio hilo zilipatikana taarifa kuwa fedha hizo
zilipotea baada ya mtuhumiwa Augustino Kayula na Frank John Mwangiba
kukamatwa akiwa na bastola aina ya Browing lakini hakuwa na fedha
zilizoporwa, na ambaye anasemekana ndiye aliyepora fedha hizo akiwa na
wenzake.
Kamanda Kova amesema pamoja na kukamatwa kwa askari hao pia wamekamatwa
majambazi wawili waliohusika na tukio hilo ambao ni ambao ni Deogratias
Kimaro mkazi wa Kilakala na Kulwa Mwakabala Mkazi wa Kijiwesamli wilaya
ya Ilala.
Watuhumiwa hao wote wanashikiliwa na upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na gwaride la utambulisho.
Chanzo: dewjiblog.com
Comments