Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi akiongea katika mkutano na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) uliolenga kupata maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Wajumbe wengine wa Tume Bi. Mary Kashonda na Bi. Salma Moulidi.
Mwananchama wa Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP) Bi. Subira Kibiga akitoa maoni ya mtandao huo kuhusu
Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo
(Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.
Wengine ni wananchama wenzake Bi. Diana Mwiru (kushoto) na Bi. Asseny
Muro.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea katika mkutano na Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP) uliolenga kupata maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya
leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es
Salaam. Kulia kwa Jaji Warioba ni Bi. Ussu Mallya, Mkurugenzi Mtendaji
wa mtandao huo, Prof. Ruth Meena 9Mjumbe wa Bodi ya TGNP) na Mwenyekiti
wa TGNP Bi. Mary Rusimbi.
Mwanachama wa Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP) Bi. Asseny Muro akitoa maoni ya mtandao huo kuhusu
Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo
(Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.
Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TGNP Bi. Mary Rusimbi na Mjumbe wa Bodi ya
mtandao huo Prof. Ruth Meena.
Comments