Chama cha Wananchi CUF kimempongeza Rais
Dk. John Pombe Magufuli kwakutatua changamoto ya ununuzi wa Korosho iliyokuwa
ikiwakabili wakulima wa zao hilo katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania.
Pongezi hizo zimeolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na
Mawasiliano Abdul Kambaya, alipozungumza na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya
CUF Jijini Dar es salaam.
“Chama cha Wananchi CUF kinampongeza Rais Dk.John Pombe
Magufuli kwa hatua aliyoichukuwa ya kununua korosho zote za wakulima, jambo
hilo ni jema kwa maslahi ya wakulima na Uchumi wa Taifa,”amesema Kambaya
Vilele Kambaya alisema Sera ya Uchumi ya Ilani ya chama chao
imeandikwa bayana jinsi itakavyo watetea wanyonge hususani wakulima nakueleza
kuwa maamuzi yaliyofanywa na Rais yana mashiko.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF
Mneke Jafari , alisema sanjari na jitihada zilizochukuliwa na Rais jitihada
zaidi zinahitajika kumkomboa mkulima kwakua ndiye anaye changia pato kubwa la
Taifa (GDP) kwa 70%.
“Ipo haja ya yakupitia upya sera na mfumo wa Wizara ya Kilimo
na Chakula ili kuepuka matatizo yanayojitokeza katika ununuzi wa mazao na
bidhaa za kilimo za aina zote, ikiwemo
uwajibishwaji wa Bodi zisizo kizi vigezo kisheria,”amesema.
Wakati huohuo Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano
Abduli Kambaya alizungumzia kuhama kwa Mbunge wa Temeke (CUF) Abdalah Mtolea na
kujiunga na Chama Cha Mapinduzi alisema CUF ipo imara.
“Hili ni vuguvugu la siasa na Mtolea siyo wa kwanza kuhama
lakini cha kushangaza hoja zakuhama kwake ni dhaifu zote ukizipitia hazina
mashiko mathalani kuhofia kufukuzwa wiki ijayo wakati hakuwa na ushahidi wa
kimaandishi kuwa angelifukuzwa,”amesema.
Vilevile Kambaya alisema miongoni mwa hoja ambazo hazina
mashiko nikuisifia CHADEMA kuwa ndiyo waliokuwa wakimpa ushirikiano kuliko CUF
na badala yake CUF imegubikwa na migogoro nakutangaza Bungeni kuwa yupo tayali
kushirikiana na Chama chochote na baada ya saa chache alijiunga na CCM.
Hata hivyo Kambaya alichambua wanasiasa wanaohama kutoka
upinzani kuelekea CCM akisema kundi la kwanza ni la Viongozi ambao bado
wanahisi wataendelea kuwa Viongozi.
Na kundi la pili alisema ni kundi ambalo haliridhiki kiuchumi
na kile wanachokipata wakiamini CCM watapatiwa nyadhifa za juu kama Ukuu wa Wilaya, Ukurugenzi wa Halmashauri,
Ukuu wa Mkoa na Ubalozi.
Kushiriki au kutokushiriki katika uchaguzi utakaofanyika
baada ya Mbunge Mtolea kuhama chama kutaamuliwa na Halmashauri ya Baraza Kuu la
CUF ndiyo lenye Mamlaka ya kuamua washiriki au laa.
Comments