Klabu za Atletico Madrid na Barcelona huenda zikapigwa faini ya Euro €3,000 hadi €6,000 kwa makosa ya utovu wa nidhamu, yaliyojitokeza kwenye mchezo wao wa Ligi uliopigwa wikiendi iliyopita.
Kamati ya ushindani ya La Liga imesema kwenye mchezo huo uliomalizika kwa klabu hizo kutoka sare ya 1-1 . Barcelona walichelewa kuingia uwanjani kipindi cha pili, huku Atletico hao mashabiki wao walirusha chupa uwanjani.
Mashabiki wa Atletico Madrid walianza kurusha chupa Uwanjani, baada ya Dembele kufunga goli la kusawazisha dakika za mwisho za mchezo huo.
Comments