KCB Bank Tanzania jana iliendesha kongamano la Biashara Club kwa mara
ya pili mwaka 2018 jijini Mwanza, Tanzania. Hii ni baada ya kuendesha
kongamano kama hili lililofana kwa wafanyabiashara zaidi ya 200 jijini
Dar es Salaam mapema mwaka huu.
Pichani ni Ms. Lightness Mlay, KCB Bank Trade Sales Manager answers questions from Mwanza business owners and executives during the KCB Bank Biashara Club Workshop held at Gold Crest Hotel in Mwanza on 29th November 2018. The event attended by more than 150 businesses in the SME sector aimed to build capacity on matters of finance management, record keeping and tax compliance.
Bi. Lightness May, Meneja wa Mauzo ya Kibiashara wa Benki ya KCB akijibu maswali kutoka kwa wafanyabiashara wa jiji la Mwanza katika hafla ya Biashara Club Workshop iliyofanyika Gold Crest Hotel tarehe 29.11.2018 jijini Mwanza. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ilikuwa na lengo la kutoa mafunzo katika maswala ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria zinazohusu kodi.
Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria
za kodi, KCB Biashara Club pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa
biashara zao kwa kuwakutanisha na wafanyabiashara wa nje na ndani ya nchi.
Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2017, KCB Biashara Club imeendelea
kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara katika seckta ya SME kwa
kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati
yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli
zao za kibiashara.
Pichani ni Mr. Abdul Juma, KCB Bank Head of SME and Mortgage speaks with Mwanza business owners and executives during the KCB Bank Biashara Club Workshop held at Gold Crest Hotel in Mwanza on 29th November 2018. The event attended by more than 150 businesses in the SME sector aimed to build capacity on matters of finance management, record keeping and tax compliance.
Nd. Abdul Juma, Mkuu wa Kitengo cha wafanyabishara wadogo na wa kati akizungumza na wafanyabiashara wa jiji la Mwanza katika hafla ya Biashara Club Workshop iliyofanyika Gold Crest Hotel tarihe 29.11.2018.
Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ilikuwa na lento la kutoa mafunzo katika maswala ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria zinazohusu kodi.
Semina hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza ilikusanya
wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, wakiwa
na changamoto mbali mbali za kibiashara zikiwemo rasilimali, ushindani,
uelewa finyu katika maswala ya kodi na nyinginezo.
Nia kubwa na
KCB Bank ikiwa ni kutaka kuwafundisha wafanyabiashara njia bora ya
kukabiliana na changamoto zinazowakumba.
Akiongea katika warsha hiyo, Meneja wa Tawi, KCB Bank Mwanza, Nd.
Emmanuel Mzava aliwashukuru wafanyabiashara na wajisiriamali kwa
kujitokeza kwa wingi kuja kupata mbinu muhimu zitakazowasaidia katika
kukabiliana na changamoto za kibiashara. “Mtegemee semina kama
hizi kwa siku za mbeleni kwani Mwanza ni jiji linaloonyesha kushamiri
kibiashara” aliongezea Nd. Mzava.
Nd. Swetbert Thomas ambaye ni mtaalamu wa mswala ya kodi
aliyealikwa na KCB Bank Tanzania mahususi kutoa mafunzo katika warsha
hiyo aliwahimiza wafanyabiashara hao kuhusu muuhimu wa kuelewa
mifumo ya kodi hapa nchini na ni kwa namna gani unagusa biashara
zao.
Mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina na safai mbalimbali
zinazoandaliwa na kitengo cha “Biashara Club”, wanachama pia
watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao ambao
utapelekea wao kuongeza si ujuzi wa kibiashara tu, bali pia kupanua
wigo wa biashara zao.
KCB Bank inatambua umuhimu wa wafanya biashara
wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia
inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao
hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.
Kuhusu Benki ya KCB
Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa
mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea
katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi
na Ethiopia.
Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii
ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala
15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika
Mashariki.
Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam,
Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya
KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua
milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika
kukuza sekta ya fedha nchini.
Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar.
Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru,Msimbazi, Lumumba, Buguruni,
Oysterbay, Mbagala jijini Dar esSalaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na
TFA, Mwanza na Morogoro.
Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi
ya 300,inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea
nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.
Comments