Vodacom Foundation kushirikiana na PSI, wamafanya tamasha liitwalo 'Kuwa Mjanja' lililolenga vijana kupata elimu ya Afya
Picha ni Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania
Foundation,Sandra Oswald (watatu kushoto) akionyeshwa na Meneja miradi
wa PSI Tanzania, Dkt. Anna Temba (wa pili kulia) ujumbe maalumu kwenye
Tablet ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia elimu ya Afya kwa vijana
wakati wa tamasha la Kuwa Mjanja lililofanyika katika shule ya Sekondari
Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo ni maalumu kwa ajili ya
vijana kupata elimu ya Afya lililoandaliwa na PSI kwa Udhamini wa Vodacom
Tanzania Foundation. Kutoka kushoto ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya
Goba Magreth Richard, Agnes John, Mhamasishaji wa Vijana PSI Semeni Likulo
na Pendo Raphael (kulia)
Picha ni Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra
Oswald (katikati ) akiwa pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Mbezi
Mwisho jijini Dar es Salaam, wakielekezwa na mtaalam wa ubunifu wa kazi za
mikono Flora Richard jinsi ya kutengeneza bangiri za batiki wakati wa
Tamasha la Kuwa Mjanja ambalo ni maalumu kwa ajili ya vijana kupata elimu ya
Afya iliyoandaliwa na PSI kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation.
Picha ni Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbezi Mwisho jijini Dar
es Salaam, wakijifunza elimu ya ujasiriamali wa kazi za mikono pamoja na
Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (
Kulia) wakati wa tamasha la Kuwa Mjanja ambalo ni maalumu kwa ajili ya
vijana kupata elimu ya Afya, elimu ya ujasiriamali iliyoandaliwa na PSI kwa
Udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation.
Tamasha hilo lilifanyika katika
Viwanja vya shule ya msingi Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam.
Comments