BARAZA la Habari Tanzania (MCT), Mtandao wa Wawatetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), na Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) umeishauri Idara ya Uhamiaji Tanzania
kutekeleza wajibu wao kwa weledi na kwa matakwa ya sheria.
Wito
huo ulitolewa jana na watetezi wa haki za binadamu jijini Dar es Salaam
kufuatia kitendo cha kukamatwa maofisa wa Kamati ya Ulinzi wa Waandishi wa
Habari (CPJ) Angela Quintal raia wa Afrika ya Kusini na Muthoki Mumo raia wa
Kenya.
Awali
akizungumza na Waandishi wa Habari Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT Pili Mtambalike,
alisema Maofisa hao wa CPJ walikamatwa na watu watatu ambao mmoja wao
alijitambulisha kuwa ni Ofisa wa Idara
ya Uhamiaji mnamo tarehe 7 mwezi huu majira ya saa 4.30 usiku katika Hotel ya
Southern Sun ya jijini Dar es Salaam.
Baada
ya kukamatwa Maofisa hao walipekuliwa, walihojiwa na kupokonywa vitendea kazi
vyao, ikiwemo komyuta mpakato, simu pamoja na hati zao za kusafiria na baadae
maofisa hao kurudishiwa vifaa vyao na kuamriwa waendelee na shughuli zao.
“Kulingana
na hofu iliyotanda kwakukamatwa kwao wadau wa Habari walifanya jitihada
kwakushirikiana na balozi za wadau hao wa Habari kurudishiwa hati zao za
kusafiria lakini balozi husika ziliwashauri kurudi makwao,”alisema
Kwa
upande wake Ofisa Programu Utetezi LHRC Raymond Kanegene alisema Waandishi hao
walikuja Tanzania kwa minajili ya kuangalia hali ya Usalama wa Waandishi wa
Habari Tanzania lakini taarifa zilizotoka kwa msemaji wa Idara ya Uhamiaji Ally
Mtanda zilisema waandishi hao walikiuka mashariti ya visa kwakuwa walipewa hati
ya matembezi.
“Cha
kusikitisha maofisa hao wakati wakukamatwa kwao hawakuambiwa sababu za
kukamatwa kwao, badae Idara ya Uhamiaji iliwachia huru pasina shariti lolote na
hivyo kuleta shaka kwao, kwamba huenda hakukuwa na sababu za msingi za
kukamatwa hivyo basi tunawaomba ndugu zetu wa uhamiaji kuwa makini,”alisema
Hata
hivyo Kanegene alisema ingetumika njia nyingine ya kushughulikia suala la
wanakamati ya CPJ kuliko njia iliyotumika na kutahadharisha kuwa haileti haiba
njema kwa mahusiano ya kimataifa kanakwamba Tanzania siyo sehemu salama.
Naye
Mratibu Taifa wa THRDC Onesmo Ngurumwa alisema watetezi wa haki za binadamu
hawakulizishwa na hatua zilizo chukuliwa dhidi ya wadau wa Habari kutoka nchi
hizo za jirani.
“Kwa
umoja wetu tunasikitishwa na namna Idara ya Uhamiaji ilivyo watendea Maofisa
hao wa CPJ kwakuwa walikuja nchini kihalali na hata kuachiwa kwao hakukua na
mashariti yoyote waliyopewa zaidi ya kuambiwa waendelee na shughuli zao, hii ni
dhahiri kuwa hawakuwa na kosa lolote ,”alisema
Kutokana
na sintofahamu iliyojitokeza waandishi wa Habari nchini wametakiwa kufanya kazi
zao kwa weledi na kufuata sheria za nchi lakini Idara ya Uhamiaji ifanye kazi
zake kwa weledi na kuzingatia mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia
ili kudumisha Amani, upendo na mshikamano.
Comments