ADB Banki yaipatia serikali kiasi cha shilingi Bilioni 486.516 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) imeipatia
Serikali ya Tanzania kiasi cha shilingi Bilioni 486.516 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akizungumza mbele ya waandidishi wa Habari mwishoni mwa wiki
wakati wa uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya fedha hizo, Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Doto James, amesema mkopo huo ni wa mashariti nafuu
ambao utarejeshwa ndani ya miaka 40.
“Mkopo huo uliombatana na msaada wa shilingi bilioni 45
zitakazo tumika katika bajeti ya maendeleo ya mwaka wa fedha 2018/19 ni matokeo
ya utawala bora na uwajibikaji wakusimamia rasilimali fedha unaotekelezwa na Serikali
ya awamu ya tano,”amesema.
Vilevile James aliitaja miradi itakayo nufaika na fedha hizo
kuwa ni mradi wa ujenzi wa Njia ya kusafirisha umeme wa msongo mkubwa (400Kv)
kuanzia Nyakanazi hadi Kigoma, mradi wakudhibiti sumukuvu, na mradi wa mpango wa kuendeleza utawala bora na maendeleo
ya sekta binafsi nchini.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkaazi wa Benki ya Maendeleo
Afrika Alex Mubiru, alisema kuwa ADB imekuewa na mahusiano na Serikali ya
Tanzania kwa mda mrefu, ni miongoni mwa nchi za kwanza kujiunga na Benki hiyo
lakini alielezea pia uwezo wa Tanzania katika utekelezaji wa miradi ya
maendeleo.
“Benki ya ADB imekuwa na mahusiano mazuri na Tanzania kuanzia
mwaka 1962 ilipoamua kuwa mwanachama katika benki hiyo na imekuwa ikichangia
michango yake kila mwaka,”amesema
Kutokana na uhusiano huo ADB imevutiwa na Tanzania na kuamua
kuipa Tanzania msaada wa shilingi bilioni 45 bila marejesho yoyote na kuahidi
kuwa itaendelea kuisadia Tanzania katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo
Mali asili na Uvuvi katika serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Ahamad Haji alisema mkopo na msaada huo umekuja wakati
muafaka nautasaidia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa pande zote
mbili.
“Ni faraja kwetu kwakuwa mkopo na msaada huu utanufaisha
pande zote mbili bara na visiwani ambapo umeme unatunufaisha wote japo ni huko
Nyakanazi, lakini udhibiti wa sumu kuvu
unatuhusu moja kwa moja, fedha hizo zitajenga maghala ya kuhifadhia nafaka na
kuboresha vituo vya utafiti na kilimo Unguja na Pemba,”amesema.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la umeme Tanzania Dk. Titus Mwinuka alisema kuwa kazi
waliyo nayo mbele yao ni kuhakikisha mradi huo mkubwa wakufua umeme unakamilika
kwa wakati.
“Kwa upande wetu wataalamu wamejipanga kuhakikisha mradi huu
una kamilika nakuunganisha Mkoa wa Kigoma kwenye Gridi ya Taifa ambapo tokea
nchi ipate Uhuru haijawahi kuunganishwa na gridi ya Taifa na badala yake
yalikuwa yakitumika mafuta ya dizeli kuendesha mitambo ya uzalishajii
umeme,”amesema.
Mradi huo wa ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme wa msongo
mkubwa kutoka Nyakanazi hadi Kigoma wenye urefu wa kilometa 280 ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa
serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa viwanda kwakujenga miundombinu
wezeshi ikiwemo umeme wa uhakika kwa gharama nafuu.
Utekelezaji wa mradi huo utahusisha upanuzi wa kituo cha
kupoza umeme cha Nyakanazi,ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme cha Kidahwe
na ununuzi wa vifaa vya uunganishaji wateja wapya wapatao 10,000 katika mkoa wa
kigoma.
Comments