Jumia ni duka pekee la mtandaoni unaloweza kuliamini kwa kufanya manunuzi ya bidhaa halisi na zenye ubora wa hali ya juu
KUELEKEA kuanza kwa msimu wa siku kuu wateja wa bidhaa za Jumia
wametangaziwa kuanza kunufaika ambapo kunzaia Novemba 16,Jumia
imezindua Black Friday kwa manunuzi ya bidhaa kwa ofa na mapunguzo
mpaka 70%.
Zawadi lukuki zitashindaniwa kila Ijumaa na kutolewa kwa punguzo
la 99% kwa wateja wa jiji la Dar es Salaam watakao fanya manunuzi
yatakayozidi shilingi 200,000 kupitia App ya Jumia pekee watape
lekewa hadi walipo bila gharama ya usafiri.
Akizungumzia kuhusu upekee wa kampeni ya Black Friday ya mwaka
huu,Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James ameeleza ,kuwa
kawaida huwa wanafanya tukio hilo kila ifikapo Novemba 23 ya
kila mwaka.
Alisema katika mwaka huu wamekuja katika hali tofauti sana
kwa sababu itakuwa ni kila Ijumaa hali hiyo inamaana kwamba
Black Friday itaanza rasmi Ijumaa hii ya Novemba 16,na itaende
lea mpaka Desemba 7.
"Tofauti na siku za kawaida,kila Ijumaa itakuwa ni ya kipekee
kwa sababu kutakuwa na ofa nyingi zaidi na mapumziko makubwa
ya bei kwa bidhaa zote mpaka kufikia 70% hii itawahakikishia
wateja kuwa hawapitwi kunufaika na manunuzi ya bidhaa kutoka
kwa wafanyabiashara tofauti wanaoaminika kwenye mtandao wetu
wa Jumia,"alisema James.
James alisema ukiachana na ofa na mapunguzo,kutakuwepo na vocha
za bure za manunuzi kuanzia shilingi 5,000 hadi shilingi 80,000
kutakuwepo na mauzo ya bidhaa ya muda mfupi katika siku(Flash
Sales).
Jumia imesema kuwa kunogesha zaidi Black Friday ya mwaka huu,
kutakuwa(Treasure Hut)kila Ijumaa ambapo bidhaa itafichwa
kwenye mtandao wa Jumia.
Hivyo mteja mwenye bahati atakayefanikiwa kuitafuta na kuipata
atauziwa kwa bei yenye punguzo la 99% yaani sawa na bure kabisa.
"Kwa mfano Ijumaa hii ya Novemba 16 ifikapo saa 9 mchana
luninga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 32 inayouzwa kwa
shilingi 570,000 mtandaoni itafichwa na itauzwa kwa shilingi
5,700 kwa mteja atakayeipata,"Alisema James.
kwa upande wake Nishit Modessa ambaye ni meneja wa tawi la
Shinyanga Emporium 1978 LTD iliyopo mtaa wa Jamhuri Dar es Salaam
aliwaambia waandishi wa habari kuwa faida ya kufanya manunuzi kwe
nye mtandao wa Jumia ni kwamba unaweza kulinganisha bidhaa kutoka
kwa wauzaji tofauti wakiwa sehemu moja,kwa kuwa bidhaa nyingi
huuzwa na muuzaji zaidi ya mmoja,kwa hiyo mteja anauhakika wa kuchagua
muuzaji mwenye bei nzuri sokoni.
Alisema angependa kutoa wito kwa watanzania kuwa werevu na kuitumia
kampeni hiyo ya Black Friday ipasavyo,kwa sababu bidhaa zozote
walizowahi kufikiria zitakuwa mbele ya macho yao kwa bei nafuu
na ofa ambazo hawakuwahi kuzitarajia.
"Kwa mfano wateja watakaofanya manunuzi yatakayozidi shilingi 200,000
kwa kutumia App ya Jumia nchini Tanzania ambayo unaweza kuipakua
kwa Google Play au App Store,watapelekewa bidhaa zao mpaka mahali
walipo bila ya gharama ya usafiri,ofa hii itakuwa ni kwa wateja
wa jijini Dar es Salaam pekee,"alisema Nishit.
Jumia ni duka pekee la mtandaoni unaloweza kuliamini kwa kufanya
manunuzi ya bidhaa halisi na zenye ubora wa hali ya juu,kupitia
mtandao wake wa www.jumia.co.tz ambapo mteja anaweza kufanya manunuzi
ya bidhaa bora na halisi muda wowote na mahali popote ulipo,mteja
pia anaweza kurudisha bidhaa endapo hatoridhika nayo ndani y7a siku 7
bila malipo yoyote na myeja anaweza lipia kwa pesa taslimu au Tigo
Pesa.
Comments