Watafiti wa masuala ya Biashara kutoka Afrika Mashariki wamesema nchi wanachama
wanapaswa kuandaa mazingira wezeshi kwa wahitimu wa vyuo vikuu ili waweze
kushiriki kikamilifu katika uchumi wa viwanda.
Wito huo umetolewa na washiriki wa Kongamano la Utafiti
wa Biashara na viwanda lililofanyika katika Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana.
Akitoa ufafanuzi kuhusu kongamano hilo Dk.Ambroz Ntika Mkuu
wa Kurugenzi ya Biashara na Ujasiriamali wa shule ya Biashara Chuo Kikuu cha
Dar es salaam alisema kongamano hilo litatoa muelekeo katika ushiriki wa watu
wote katika uchumi wa viwanda.
“Serikali iandae mazingira wezeshi ambapo wanafunzi wetu
kuanzia ngazi ya chini wanapohitimu waweze kujitegemea na siyo kusubiri
kuajiriwa kwakufanya hivyo tutatengeneza ajira nyingi na pato la kaya na Taifa
litaimarika,’alisema.
Washiriki wa Kongamano hilo watadadavua mada 12 muhimu
nakuzitolea maamuzi nakuzipeleka kwa watunga sera katika serikali za nchi
wananchama ili kufanyiwa kazi ambapo mada 35 zitawasilishwa.
Dk.Ntika alisema mkutano huo kwa Tanzania umekuja wakati
muafaka ambapo zaidi ya viwanda 3000 vya kati na vidogo vimeanzishwa ndani ya
miaka mitau ya utawala wa Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Kwa upande wake Profesa Isaack Mbeche kutoka shule ya
Biashara Chuo Kikuu cha Nairobi alisema wamekutana ili kuchambua tafiti
walizozifanya nakuziwasilisha katika idara mbalimbali kwa nchi wanachama ili
zifanyiwe kazi.
Hata hivyo Uhuru lilitaka kujua je tafiti hizo zinafanyiwa
kazi ipasavyo au zinakusanywa na kisha kuwekwa kwenye kabati,akijibu swali hilo
Profesa Mbeche alikiri kuwa kuna uzembe katika serikali za nchi wanachama kwa
kisingizo cha kukosekana rasilimali fedha.
“Ni ukweli usiopingika kuwa tunaandika maandiko mengi na
tafiti nyingi lakini suala la utekelezaji lina kuwa na ukwakwasi na wakati
mwingine shida haipo mamlaka za juu lahasha utakuta mkuu wa idara anakwamisha
utekelezaji bila sababu za msingi zaidi atakuambia fedha hakuna.
Hata hivyo Profesa Mbeche alishauri ili tuweze kuimarisha
viwanda vya ndani nchi wanachama hawana budi kulinda viwanda hivyo kwakununua
bidhaa za ndani na kupenda bidhaa za nchi wanachama lakini wakitakiwa kuzalisha
bidhaa zenye ubora.
Mmoja wa washiriki wa Kongamano hilo ambaye pia ni mwanafunzi
wa mwaka watatu akichukua shahada ya Biashara chuoni hapo Geoffrey Mwamanga
aliliambia Uhuru ili soko la ndani na viwanda viweze kushamiri sula la sarafu
moja na soko la pamoja ni muhimu kwa wakati huu.
“Kinadharia tunaambiwa kuna soko la pamoja limeanza lakini
binafsi sioni kimatendo kwakua hatuna sarafu moja kama wenzetu huko ulaya hapa
nnachoshudia ni makongamano tu na maonesho ya kimataifa ya Biashara mara jua
kali au sabasaba,”alisema.
Kongamano hilo ni la 14 kufanyika nchini na Kongamano
linguine litafanyika nchini Uganda mwaka 2019.
Comments