Azam FC maarufu kama wana lambalamba wameanza rasmi mazoezi tayari kuanza
safari ya kuzisaka pointi kuelekea mchezo ujao dhidi ya Stand United.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utafanyika kwenye Uwanja
wa Azam Complex Desemba 4 mwaka huu, ambapo Azam FC iko kwenye mwenendo
mzuri baada ya kushinda mechi saba mfululizo za ligi hiyo.
Wachezaji wote wa Azam FC wameripoti mazoezini wakiwa na hali nzuri
kabisa isipokuwa kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, ambaye ni mgonjwa.
Beki wa kulia Nickolas Wadada, aliyekuwa kwenye majukumu ya timu ya
Taifa ya Uganda, naye amesharejea kundini akiwa ni miongoni mwa
wachezaji walioripoti kwenye mazoezi hayo.
Kikosi cha Azam FC kinatarajia kuendelea na mazoezi kwa wiki hii
yote, na siku ya Jumamosi wanatajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu
ya vijana ya timu hiyo (Azam U-20) kwa ajili ya kujiweka sawa
utakaopigwa asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex..
Azam FC inayonolewa na Kocha Mholanzi Hans Van De Pluijm akisaidiana
na Juma Mwambusi hadi sasa imeshacheza mechi 13 za ligi, ikiwa
imesdhinda mara 10 na kutoka sare mara tatu ikijikusanyia jumla ya
pointi 33 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikifuatiwa na Yanga
wenye alama 32 tayari kwakicheza michezo 12 wakishinda 10 wakitoka sare
mara 2.
Na katika dirisha la Usajili lililofunguliwa Novemba 15, Azam
wameshafanikiwa kunasa saini ya Mshamuliaji wa Kimataifa wa Zambia Obrey
Chirwa huku ikiwaotoa wachezaj wake Ditram Nchimbi, Mbaraka Yusuf
kutolewa kwa mkopo.
Comments