Rais wa Marekani Donald Trump amesema amejuzwa kuhusu mkanda wa sauti wa mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi lakini amesema binafsi hatousikiliza.
"Ni mkanda wa maumivu, ni mkanda mbaya," Trump ameiambia runinga ya Fox News.
Shirika la ujasusi la Marekani CIA linaaminika kufikia kikomo kuwa mwanamfalme Mohammed bin Salman aliamrisha kutekelezwa kwa maujai hayo, japo bado Ikulu ya White House haijathibitisha uchunguzi huo.
Saudi Arabia imeziita taarifa hizo kuwa ni za uongo na kudai kuwa bin Salman hakuwa na taarifa yoyote juu ya kutekelezwa kwa mkasa huo.
Khashoggi, alikuwa ni kinara wa kuukosoa utawala wa kifalme wa Saudia. Aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul Oktoba 2 alipoenda kuchukua karatasi zake za talaka.
Saudia inasema aliuawa katika operesheni haramu iliyotekelezwa na maafisa wake wa usalama.
Hata wanaomuunga mkono Trump ndani ya Bunge la Wawakilishi wanamtaka achukue hatua kali juu ya mauaji hayo. Lakini kutokana na unyeti wa Saudia kama mshirika thabiti wa Marekani katika Mashariki ya Kati kunamfanya Trump kuwa mgumu katika kufanya maamuzi.
Mwanamfalme wa Saudia aliamini 'Khashoggi alikuwa hatari'
Trump amesema hana haja ya kusikiliza sababu ameshaelezwa juu ya maudhui ya mkanda huo.
"Ninafahamu kila kitu kilichomo ndani ya mkanda bila hata ya kuusikiliza," aliiambia Fox katika mahojiano yaliyorushwa jana Jumapili Novemba 18. "Iikuwa ni vurumai, uovu mkubwa na mbaya sana."
Katika mahojiano hayo, Tump amesema Mohammed bin Salman amemwambia kuwa alikuwa hajui lolote juu ya mpango na kutekelezwa kwa mauaji hayo.
Trump amedai kuwa yawezekana isijulikane kabisa nani alikuwa nyuma ya mauaji hayo, hata hivyo amesema tayari kuna vikwazo vimeshawekwa juu ya wale wanaoshukiwa kutekelza uovu huo.
"Lakini wakati huo huo tunaye mshirika na mimi nataka nishikamane na mshirika ambaye kwa namna nyingi tu amekuwa mwema," amesema Trump.
Hata hivyo, mahojiano ya Trump na Fox yalifanyika kabla ya kuvuja kwa ripoti ya CIA.
Japo CIA hawakutoa ushahidi wa moja kwa moja juu ya uhusika wa bin Salman to the murder, maofisa wa shirika hilo wanaamini tukio kama hilo lisingeweza kufanyika bila ruhusa yake.
Jumamosi, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema haijafikia hitimisho juu ya mauaji hayo, ikisema kuna maswali mengi ambayo hayajapata majibu.
Jana Jumapili Trump amesema serikali yake lazima ifanye maamuzi.
"Tutakuwa na ripoti kamili ndani ya siku mbili, yawezekana Jumatatu au Jumanne," amesema Trump. Kwa msaada wa BBC Swahili.

Comments