HATIMAYE kile kitendawili cha muda mrefu cha Nani ata twaa taji la Redds
Miss Tanzania 2012, kimeteguliwa usiku wa Novemba 3, 2012, baada ya
Mrembo kutoka Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam, Brigitte Alfred kutwaa taji hilo.
Brigitte ambaye nyota yake katika mashindano hayo ya urembo nchini
ilianza kung’aa tangu Kitongoji cha Sinza baada ya kutwaa taji la Sinza
na Baade kutwaa Taji la Redds Miss Kinondoni amedhihirisha ukali wake
baada ya kuwabwaga warembo wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo
kutoka Kanda mbambali.
Mpinzani mkubwa wa Brigitte katika shindano hilo alikuwa ni Mrembo
kutoka Kanda ya Ziwa ambaye nae alianza kuwika baada ya kutwaa taji la
Redds Mkoa wa Mara na baade kutwaa taji la Kanda ya Ziwa, Eugene Fabian.
Enagene alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika shindano hilo kubwa
ambalo Brigitte ameondoka akiendesha gari aina ya NOAH na kitita cha
Shilingi Milioni 8.
Nafasi ya tatu ilikwende kwa Malkia wa Kitongoji cha Kigamboni City na
Miss Temeke 2012, Edda Sylvesta huku nafasi ya Nne ikichukuliwa na
Mrembo wa Dar Indian Ocean na Kinondoni, Magdalena Roy na nafasi ya Tano
ikienda Kanda ya Ziwa tena kwa Mkoa wa Mwanza, Happyness Daniel.
Brigitte Alfred akipunga mkono kwa furaha mara baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi na kuwabwaga washiriki wenzake 29.
Mshindi
wa Taji la Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati)
akipunga mkono kwa furaha katika picha ya pamoja na mshindi wa Pili,
Eugene Fabian (kushoto) na Mshindi wa Tatu, Edda Sylvester mara baada ya
warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo. Brigitte
anatokea Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni wakati, Eugene
anatoka Mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa huku Edda ni Miss Kigamboni na
Kanda ya Temeke.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatu5 bora ya Redds Miss Tanzania 2012,
kutoka kushoto ni Brigitte Alfred, Eugen Fabian, Happyness Daniel, Edda
Sylvester na Magdalene Roy wakipozi kwa picha.
Kwa taswira zaidi http://mrokim.blogspot.com
Comments