SAKATA ya mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha
Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi limeendelea kuchukua
sura mpya mkoani Iringa baada ya askari polisi anayetuhumiwa
kuhusika na mauwaji hayo kufichwa katika gari maalum na askari wenzao
Askari polisi wakiweka ulinzi kumziba mwenzao asipigwe picha leo
Tukio hilo lilitokea leo wakati mtuhumiwa huyo akifikishwa mahakamani
huku askari polisi hao muda wote walionekana kuzunguka huku na kule
katika mahakama hiyo kama njia ya kuwathibiti wanahabari waliokuwepo
mahakamani hapo wasipate nafasi ya kumpiga picha mtuhumiwa huyo
ambaye ni askari mwenzao mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni
(23)
Hata hivyo kabla ya kuingia karandika la mahabusu wengine gari ya
polisi aina ya Toyota yenye namba za usajili PT 1404 ikiwa na askari
zaidi ya 10 ilifika katika viwanja hivyo vya mahakama na kuegeshwa
pembeni bila ya mtuhumiwa huyo aliyekuwa amefunikwa sura yake kwa
kofia na kufichwa kabisa sura yake kuonekana huku akiwa amekaa mbele
kwa dereva huku akifichwa na askari mwenzake pasipo kushuka.
Zikiwa zimebaki kama dakika 10 mahakama kuanza gari hilo lilisogea
hadi mlango wa Mahakama na askari waliokuwepo mahakamani hapo zaidi ya
20 kulizunguka gari hilo huku wengine wakiwathibiti wanahabari
akiwemo mwandishi wa habari hizi kama njia ya kuzuia kupigwa picha kwa
mtuhumiwa huyo na baada ya kuingia ndani ya mahakama kabla ya hakimu
kufika uthibiti ndani ya chumba cha mahakama ulikuwa mkali zaidi dhidi
ya wanahabari hasa wale wenye kamera.
Wakati huo huo Mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa
imeahirisha kesi hiyo ya mauwaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi ambae
pia alikuwa ni mwenyekiti klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa
(IPC) ,mtuhumiwa huyo askari mwenye namba G2573 Simoni (23)
atafikishwa tena mahakamani hapo Desemba 5 mwaka huu kesi hiyo itakapo
tajwa tena.
Mwendesha mashitaka wa jamhuri Adolf Maganda aliieleza mnahakamani
hiyo mbele ya hakimu Dyness Lyimo kuwa mtuhumiwa huyo mnamo 02
Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa
Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria
namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.
Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16
iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya
kukusudia kupewa dhamana.
Chanzo: francisgodwin.blogspot.com
Comments