Mkurugenzi wa shindano hayo, Methuselah Magese akizungumza mbele ya
waandishi wa habari (hawapo pichani).
SHINDANO la kusaka wanamitindo wenye vegezo vya
kipekee nchini, linaloratibiwa na kampuni ya Unique Entertainment, leo
limezinduliwa rasmi katika hoteli ya Holiday Inn Posta jijini Dar es Salaam.
Magese (katikati) akiwa pamoja na bodi yake ya
uandaaji…
Shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye vigezo vya kipekee
nchini Tanzania(unique model) linaloandaliwa na Unique Entertainment
limezinduliwa leo jumatano kwa kishindo katika hoteli ya Holiday Inn iliyopo
katika ya jiji la Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa habari hao katika ufunguzi huo mkurugenzi wa
shindano hilo Bw.Methuselah Magese amesema kuwa mchakato wa shindano
umefunguliwa rasmi ili kutoa fursa ya wadhamini kujitokeza kwa wingi kudhamini
shindano hilo ambalo litakuwa na mvuto wa aina yake kwa msimu huu wa pili.
Pia wanamitindo wenye sifa za kimataifa wameombwa kujitokeza kwa wingi
katika usaili utakaofanyika tarehe 18 novemba katika hoteli ya Lamada
Apartments.
Tumeboresha shindano kwa kiwango cha hali ya juu tofauti na ilivyokuwa
hapo awali,lengo ni kulifanya shndano hili liwe la heshima,hadhi na
linalotimiza lengo lake la kuvumbua na kuinua vipaji vya wanamitindo wa
kchipikizi.
“Tunaomba wabunifu wadogo kwa wakubwa wajitokeze kuja kuonyesha umahili
wao katika shindano hili ambapo mwaka huu tutakutanisha wabunifu wengi wa
mavazi nchini Tanzania katika shindano moja kwa lengo la kuwainua wabunifu
wadogo na kuendelea kuwatangaza wabunifu wenye majina makubwa katika tasnia ya
mitindo hasa katika kipindi hiki maridhawa cha mwisho wa mwaka” alisisitiza
Magese.
Katika msimu huu wa pili wa unique model kutakuwa na nyongeza ya mataji
mengine madogo matatu amabayo ni “model photogenic 2012”,”model talent 2012” na
“model with good manner 2012” ambapo mataji hayo yatakuwa chini ya taji kuu la
“Unique model of a year 2012”.
Fainali za shindano la Unique model 2012 zitafanyika mwishoni mwa mwezi
Desemba ambapo kamati ya maandalizi imedhamilia kufanya onyesho lenye hadhi
kuanzia ubora wa washiriki wenye vigezo vya uanamitindo ambao wataleta
mabadiliko katika tasnia ya mitindo nchini.
Shindano la Unique model lilianzishwa mwaka 2010 ambapo kwa mwaka huu ni
mara ya pili kufanyika,Asia Dachi ndiye mwanamitindo anaeshikilia taji hilo
mpaka sasa.
Wito umetolewa kwa makampuni kujitokeza kuchukua mabalozi ambao ni
wanamitindo washiriki kwa lengo la kufanya nao kazi za kutangaza bidhaa ama
huduma inayotolewa na kampuni husika kwa lengo la kutoa ajira kwa wanamitindo
hao wanaochipukia katika tasnia.
Unique model 2012 imedhaminiwa na Dtv,Gazeti la Tanzania Daima,Mashujaa
investment ltd,Sophernner Investment co ltd,K.d.surelia,young don records,Kiu
investment ltd,Oriental bureau de change,100.5 Times fm,J’s professional
ltd,Lamada apartments hotel, na Unique entertainment blog.
Comments