Fred alianza kazi ya utangazaji katika Radio Tanzania kabla ya kwenda Ulaya kwa mafunzo.
Amekuwa akifanya kazi ulaya akiendelea na masomo
ya shahada ya pili ya masters kwenye digital media katika chuo kikuu
kimoja cha London.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata
sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi
wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.
Alishiriki pia katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC
wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na anayepatana na
wote, na ambaye alikuwa mtangazaji tulivu na akishikilia kazi lazima
ahakikishe kuwa ameimaliza vema iwezekanavyo.
Matayarisho yanafanywa kusafirisha mwili wake hadi Tanzania
Chanzo: BBC- SWAHILI./http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
Comments