Mkurugenzi
wa kampuni ya QS, Mhonda Entertainment, Josefh B. Mhonda (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ujio wa JB
Mpiana.. Kulia ni Rais wa bendi ya Mashujaa, Chalz Baba.
Meneja wa JB Mpiana, Guyguy Kiangala,akielezea ujio wa mwanamuziki huyo kuja kufanya onyesho hapa Tanzania.
KAMPUNI ya QS ya jijini inatarajia kumleta nchini mwanamuziki
nguli wa Jahmuri ya Kidemokrais ya Congo, JB Mpiana wa bendi ya Wenge
BCBG katika uzindizi wa bendi ya Mashujaa Musica ya jijini unaotarajia
kufanyika katika viwanja vya Leaders November 30 mwaka huu.Bendi hiyo ya Mashujaa inatarajiwa kuzindua albam yao ya ‘Risasi Kidole’ yenye nyimbo sita. Burudani zingine zitakazokuwepo siku hiyo ni wanamuziki wa kizazi kipya ambao ni H. Baba, Ney wa Mitego, Mb Dog na wasanii wengine kibao wa muziki wa kizazi kipya.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/GPL)
Comments